Mfuko wa Pensheni wa PPF upo katika Viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi katika Maonesho ya Nane nane ili Kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya Mfumo wa WOTE SCHEME kwa Sekta Binafsi kama Vile Wakulima,Wafugaji, Mama Lishe, Madereva Bodaboda na Wajasilamali mbalimbali ili waweze kujiwekea Akiba wakati huohuo wakinufaika na Bima ya Afya, Mikopo kwa Ajili ya Kujiendeleza Kielimu, Kuongeza Mtaji na Kunufaika na Pensheni za kila Mwezi.
Akiongea, Bi Janeth ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutembelea Banda hilo la PPF kwa ajili kupata elimu na kujiunga na mfuko huo na kufaidika na fursa zinazotolewa na PPF.
Baadhi
ya Wananchi wakijaza Fomu ya Kujiunga na WOTE SCHEME katika Banda la
PPF Viwanja vya Nane Nane Ngongo Kama Picha Inavyoonekana Afisa Uhusiano
Mwandamizi, Janet Ezekiel akitoa maelekezo ya Jinsi ya Kujaza Fomu
Hizo.
Baadhi
ya Wananchi wakijaza Fomu ya Kujiunga na WOTE SCHEME katika Banda la
PPF Viwanja vya Nane Nane Ngongo Kama Picha Inavyoonekana Afisa Uhusiano
Mwandamizi, Janet Ezekiel na Afisa Masoko PPF, Wakitoa maelekezo ya
Jinsi ya Kujaza Fomu Hizo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi, Janet Ezekiel akimkabidhi kadi ya WOTE SCHEME kwa mwananchi aliyejiunga na Mfuko huo.
Wananchi waliotembelea Banda la PPF, wakimsikiliza kwa Makini Afisa Masoko PPF Wakati akitoa Elimu Juu ya Mfumo wa WOTE SCHEME.

No comments:
Post a Comment