HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 17, 2016

VIDEO: HAYA NDIO MAGOLI YA PENATI YA AZAM NA YANGA UWANJA WA TAIFA LEO

Mgeni Rasmi katika Mtanganye wa kuwania Ngao ya Jamii uliozikutanisha Timu ya Azam na Yanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akikabidhi Ngao hiyo kwa Nahodha wa Timu ya Azam, John Boko 'Adebayour', baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-1, kufuatia mchezo wao kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Wachezaji wa Timu ya Azam pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa Ngao ya Jamii, kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-1, kufuatia mchezo wao kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Kipa wa Azam, Aishi Manula akiruka kuwania mpira uliopigwa na Mchezaji wa Yanga, Haruna Niyonzima ambao ulikwenda nje wakati wa changamoto ya mikwaju ya penati kuamua nani wa kunyangua Ngao ya Jamii, ambayo imekwenda wa Timu ya Azam, baada ya kuichabanga Yanga mabao 4-1 kufuatia mchezo wao kumalizika kwa sare ya bao 2-2.
Kipa wa Yanga, Deogratius Munish akiwa kapelekwa markiti kwa Mkwaju wa penati ulioimaliza Yanga, uliopigwa na Mchezaji wa Azam, Bolou Kipre.
Wachezaji wa Timu ya Azam, wakishangilia Ushindi wao kwa kumrusha juu juu Kocha wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad