Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiangalia Makabrasha kutoka
Kampuni ya State Grid ya China ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa njia ya
umeme ya Msongo wa kV 400 ya Mchuchuma hadi Makambako.
Kampuni ya State Grid ya China imeonesha nia ya kuwekeza katika Mradi wa Kujenga Njia ya umeme ya
Msongo wa kV 400 ya kutoka Mchuchuma hadi Makambako.
Hayo yamebainika katika kikao kati ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Balozi
wa China nchini, Dkt Lu Youqing aliyeambatana na ujumbe huo wa kampuni hiyo.
Profesa Muhongo alichukua fursa hiyo kuieleza kampuni hiyo kuhusu Hazina iliyopo nchini ya Makaa ya
Mawe na kusema kuwa, bado Serikali inatafuta wawekezaji ambao watazalisha umeme kwa kutumia
chanzo hicho na kuongeza kuwa, “Bado tunahitaji wawekezaji kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya
mawe”.
Aidha, mbali na kuonesha nia ya kuwekeza katika Mradi huo, Kampuni hiyo imefika Wizarani kutaka
kujua maeneo mengine ya uwekezaji katika sekta ya Nishati ambayo kampuni hiyo inaweza kufanya kazi
nchini.
Vilevile, kampuni hiyo ilimweleza Waziri uzoefu ilionao katika shughuli hizo na kuzitaja baadhi ya nchi
ambazo inatekeleza miradi kama hiyo kuwa barani Afrika kuwa ni pamoja na Ethiopia, Egypt, Kenya na
Afrika Kusini.
Waziri wa Nishati na Madini (katikati) Profesa Sospeter Muhongo akiwaeleza jambo Balozi wa China
nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake waliofika Ofisini kwa Waziri ili kufahamu
namna kampuni hiyo inavyoweza kufanya kazi katika sekta ya Nishati nchini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao baina
yake na Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake waliofika Ofisini
kwa Waziri ili kufahamu namna kampuni ya State Grid ya China inavyoweza kufanya kazi katika sekta ya
Nishati nchini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza Mwakilishi wa Kampuni ya
State Grid ya China upande wa Afrika, Mingu Liu, (wa kwanza kulia mbele) wakati akimweleza Waziri
Muhongo azma ya Kampuni hiyo kuwekeza katika Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme ya Msongo wa kV
400 Mchuchuma hadi Makambako. Wengine wanaofuatilia ni Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na
ujumbe wake.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikakti) na Balozi wa China nchini Dkt. Lu
Youging (wa pili kushoto) na ujumbe wake wakifurahia jambo mara baada ya kumalizika kwa kikao baina
ya Waziri, Balozi na kampuni ya State Grid.
No comments:
Post a Comment