HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 21, 2016

Mwanariadha wa mbio ndefu wa Tanzania ashika nafasi ya tano kwenye Olympic huko Rio, Brazil

 Mwanariadha wa mbio ndefu wa Tanzania Alphonce Felix Simbu (24) leo ametia fora kwa kushika nafasi ya 5 kwenye siku
ya mwisho ya michuano ya Olimpiki katika mashindano ya marathon jijini Rio de Janeiro nchini Brazil. Alitumia saa 2:11:15, sekunde 11 nyuma ya mshindi wa nne Ghirmay Ghebreslassie.
Mkenya Eliud Kipchoge ndiye aliyeibuka mshindi na kunyakuwa medali ya dhahabu katika mbio za marathon upande wa wanaume. Feyisa Lilesa wa Ethiopia alimaliza wa pili akiwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde 70 na  kushinda medali ya fedha huku Mmarekani Galen Rupp akimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad