HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 16, 2016

JE YANGA KUENDELEZA UBABE KWA AZAM?

Na Zaina  Nyamka, Globu ha Jamii.
IKIWA Yanga wanahitaji kuendelea kunyakua Ngao ya Hisani kwa mara ya nne mfululizo na wakiwa tayari wameshanyakua mara sita, timu ya Azam nayo imejizatiti kuhakikisha mara hii wanachukua kwa mara ya kwanza.

Katika historia ya timu hizo mbili zimekutana mara 25, Yang ikifanikiwa kushinda mara 10 Azam wakishinda mara nane wakienda sare mara saba.

Yanga wamefanikiwa kuifunga Azam mara tatu mfululizo katika mchezo wa ufunguziwa ligi yaani Ngao ya Hisani na kufanikiwa kulinyakua mara tatu mfululizo kombe hilo.
Benchi la ufundi la Yanga, likiwa chini ya Mholanzi Hans Van De Pluijm anakutana na Azam kwa mara ya pili mfululizo  huku Azam wakiw chini ya benchi jipya la makocha kutoka nchini Hispania.

Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas ametangaza viingilio vya mchezo huo ni 5000 kwa viti vya bului, Kijani na machungwa, VIP B /C ni 15000 huku VIP A itakuwa ni 20000 na katika mapato ya mchezo huo kiasi cha fedha kitakachopatikana kitanunua madawati 200 na kuyapeleka kwenge Ofisi za Bunge na kumkabidhi Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Thomas Kashilila.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 10 alasiri katika dimba la uwanja wa Taifa unatarajiwa kuonyeshwa na kituo cha Televisheni cha ATN baada ya kupata haki za kurusha matangazo ya mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad