HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 26, 2016

AFISA MIFUGO ASIMAMISHWA KAZI KWA UZEMBE

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi amemsimamisha kazi Afisa Mifugo wa Kata ya Chitego kwa uzembe ulokithili nakutokujali, lakini pia dharau kwa wafugaji na Hatimae kupoteza Ng'ombe zaidi 50 na ndani ya Mwaka huu.

Ndejembi alifika Mapema Katani hapo nakuanzia Ofisi ya Kata nakusaini kitabu kisha kufanya Mkutano wa Hadhala na Wanakijiji hao ambao kwa Wingi wao walikuwa ni Wakulima.

DC aliongea na Kusikiliza Kero za Wananchi hao, nakuzitatua papo hapo kwa kushauriana na Wananchi na Viongozi wao, hali iyomlazimu kufanya ziara hiyo baada ya Ng'ombe zaidi ya 12 kufa juzi kwa kulishwa Sumu.

Kitendo ambacho wafugaji walimpigia simu Afisa Mifugo ili aje kusaidia Kuokoa Uhai wa mifugo hiyo Lakini hakufika Licha yakuwa anaishi Ndani ya Kata hiyo hiyo, Kilichowakera wananchi zaidi ni Afisa huyo kutokufika lakini Mtendaji na Baadhi ya Viongozi walifika ktk Eneo la Tukio.
Malalamiko ni Pamoja na Afisa Mifugo kuwatukana nakutokujali Uhai wa Mifugo ya wafugaji hao.

Hivyo DC Ndejembi alisikiliza yote pande zote na Hatimae kufikia Uamuzi wa Kumsimamisha Afisa Mifugo kwa uzembe wake, Kwani Ndani ya Mwaka huu Ng'ombe zaidi ya 35 wamekufa na yeye hakuonyesha kujali zaidi ya Kuleta Dhalau kwa Wafugaji hao.
DC ameomba Afisa Mifugo huyo atafutiwe mahala pakufanya kazi ambako patamfaa kwa sasa!

Tayali watuhumiwa 5 wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi. Na migogoro hii wananchi wenyewe wamekiri kuwa wanayumbishwa na viongozi wao wa kata, na kuna tabia za Siasa Chafu zinaendelea ktk Kata hiyo.

Wanakijiji hao walitakiwa kutomfumbia Macho mtu yeyote ambae atakua mzembe na Atakaekiuka Taratibu, Kanuni na Sheria ya Nchi, atatendewa haki yake ya kimsingi kwa kuadhibiwa kama kakosa ili kutoa funzo kwa jamii ya watanzania nakujifunza uwajibikaji kwa kila ngazi aliyonayo Mtumishi wa serikali.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akiwa na baadhi ya wananchi wake wa Jamii ya Wafugaji.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akizungumza na Afisa Mifugo wa Kata ya Chitego.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad