Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (watatu kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser (wapili kulia) pamoja na ujumbe wake mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyojadili ushirikiano katika masuala ya kuhudumia wakimbizi nchini. Kikao hicho kilifanyika wizarani, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimsalimia
Naibu Katibu Msaidizi wa Idara ya Inayoshughulikia Idadi ya Watu,
Wakimbizi na Uhamiaji ya nchini Marekani, Catherine Wiesner wakati
ujumbe huo ambao uliongozwa na Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia
Blaser (watatu kushoto). Kikao hicho kilichofanya katika Ukumbi mdogo
wa Wizara, jijini Dar es Salaam kilijadili ushirikiano katika masuala ya
kuhudumia wakimbizi nchini. Wapili kushoto ni Balozi wa Marekani katika
Umoja wa Mataifa-Geneva, Pamela Hamamoto.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akizungumza na
Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser (wa pili kulia) pamoja
na ujumbe wake katika kikao kilichofanya katika Ukumbi wa Wizara hiyo,
jijini Dar es Salaam ambacho kilijadili ushirikiano katika masuala ya
kuhudumia wakimbizi nchini. Watatu kulia ni Balozi wa Marekani katika
Umoja wa Mataifa-Geneva, Pamela Hamamoto na anayefuata ni Naibu Katibu
Msaidizi wa Idara ya Inayoshughulikia Idadi ya Watu, Wakimbizi na
Uhamiaji ya nchini Marekani, Catherine Wiesner. Kushoto ni Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akiandika
maelezo ya Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser (katikati)
katika kikao cha kujadili ushirikiano katika masuala ya kuhudumia
wakimbizi nchini. Kushoto ni Balozi wa Marekani katika Umoja wa
Mataifa-Geneva, Pamela Hamamoto. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi
mdogo wa Wizara, jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment