HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 3, 2016

WATOTO WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA NEW HOPE FAMILY WAPATA MSAADA WA BAISKELI KWA AJILI YA USAFIRI WA SHULENI

Mama mlezi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe 11, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Asha Juma akiwapa maelezo wafanyakazi wa woolworths wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Joehans Mgimba (aliyeshika mtoto) juu ya kituo hicho wakati walipowapelekea msaada wa beiskeli na Vyakula mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya Woolworths nchini, Joehans Mgimba akiwa amembeba mtoto Noline Gifti ,wakati walipokwenda kutoa msaada wa vyakula na baiskeli kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe two, Kigamboni jijini Dar es Salaam.wengine kutoka kushoto niMkuu wa Operesheni, Anna Grace Cussack na Mkuu wa Duka hilo Mikocheni, Frank Ngoni.
Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya Woolrths nchini, Joehans Mgimba akiwa amembeba mtoto Noline Gifti (kushoto) na Mkuu wa Fedha Samson Katemi wakicheza na mtoto Noline wa kituo cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe two, Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Operesheni, Anna Grace Cussack.
Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya woolworths nchini ,Joehans Mgimba akisalimiana na baadhi ya  Watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family Group, kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa Kampuni hiyo walipokwenda kutoa msaada wa Baiskeli na Vyakula mbalimbali kituoni hapo.Kulia ni mkuu wa fedha Samson Katemi.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Kulelea watoto waishio katika mazingira hatarishi cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaamwakisukuma beiskari pamoja na Wafanyakazi wa Woolworths wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Joehans Mgimba,mara baada ya kukabidhiwa msaada huo pamoja na vyakula na kampuni hiyo.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaamwa wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Woolworths, mara baada ya kukabidhiwa msaada wa baiskeli na vyakula mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa maduka ya Woolworths nchini, Joehans Mgimba akiwa amempakia kwenye baiskeli kijana Majaliwa Anthony, ambaye ni miongoni mwa Watoto wanaolelewa katika kituo cha New Hope Family Group Kilichopo Mwasonga Kata ya Kisarawe , Kigamboni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya kuonyesha jinsi watoto hao watakavyokuwa wanabebana wakati wa kwenda shule ili kuwahi masomo.kampuni hiyo ilitoa msaada wa baiskeri na vyakula mbalimbali kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad