HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 5, 2016

WASHINDI WA TUSKER FANYA KWELI UWINI WAZIDI KUONGEZEKA



Meneja mauzo wa eneo la Sinza John Nyaguti(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mmoja wa washindi wa promosheni ya Tusker Fanya Kweli Uwini Grace Richard(kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika Sinza jijini Dar es Salaam.


Zaidi ya Milioni 70 zimetolewa kwa watumiaji wa bia ya Tusker nchi nzima mpaka sasa!

 Watumiaji wa bia ya Tusker waendelea kutabasamu huku wengine kumi wamejishindia mamilioni leo ambapo kila mmoja amejinyakulia Milioni moja kutoka katika promosheni inayoendelea ijulikanayo kama Tusker Fanya Kweli Uwini. 
Tayari rekodi ya washindi 60 kutoka sehemu mbalimbali nchini wameshajishindia Milioni moja kila mmoja kutoka katika droo za wiki zinazofanyika kila Ijumaa na tayari wameshapokea pesa zao. Ili kuwa sehemu ya droo, kuponi au vocha zilikusanywa kutoka bar mbalimbali nchi nzima na droo kurekodiwa ambapo washindi wengine kumi wametangazwa.

Droo ya sita iliyofanyika na kurushwa na kituo cha ITV ilishuhudiwa na Afisa mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini ambaye huhakiki na kusimamia droo iweze kuendeshwa kulingana na taratibu zilizowekwa, wakaguzi wa nje na washirika mbalimbali. 
Wafuatao walitangazwa washindi wa droo ya sita ya Tusker Fanya Kweli Uwini:- Sharifa Samuel na Aisha Watanga kutoka Pwani, Inai Ngw’avi na Cleophance Faostine kutoka Dar es Salaam, Emmy Lakanga kutoka Iringa, Keneth Mwenda kutoka Morogoro, Simon Mrema kutoka Aruska, John Mhina kutoka Tnga, Pili John kutoka Mwanza na Neema Charles kutoka Shinyanga.

Akizungumza wakati wa droo hiyo Meneja wa Bia ya Tusker Jasper Maston alisema ushiriki bado upo vizuri na jinsi siku zinavyoenda washiriki wanazidi kuongezeka hata kama kampeni yetu inaelekea ukingoni watumiaji wengi wa bia ya Tusker bado wanashauku kubwa ya kuwa katika mashindano hayo. 
“Bado tuna wiki chache tu kufikia mwisho wa promosheni yetu lakini chakushangaza tumepata mrejesho mzuri kutoka kwa wateja wetu, bado tunawatia moyo watumiaji wa bia ya Tusker waendelee kushiriki mara nyingi wawezavyo kwani kushiriki mara nyingi kunawaongezea nafasi ya ushindi” alisema Maston.

Washindi wa Tusker Fanya Kweli Uwini wamekua mstari wa mbele kuzungumzia mambo mazuri waliyopata kutoka na promosheni hiyo. Katika ziara ya kushtukiza Mbezi Luis, mwenye furaha ya kupitiliza Grace Richard alisema anabahati sana kushiriki. “Tangu promosheni hii imeanza nimekua nikiangalia droo zote kupitia Televisheni na mwisho wa siku nikajiuliza, kwanini na mimi nisishiriki katika hii promosheni? Kwa bia moja na kuponi moja tu, Nimeshinda. Sikuamini siku nimetangazwa kuwa moja ya washindi wiki mbili zilizopita” alisema Grace.

Pia aliongeza kuwa amekutana na wanawake wenzake wakati wa hafla ya makabidhiano na hivyo kumfanya ajisikie huru zaidi na mazingira hayo ingawa ilikua mbali na mahali anapoishi. “Muda mwingine huwa ni vigumu sana kwa sisi wanawake kushiriki katikapromosheni za pombe, lakini nafurahi nilishiriki na sasa nimepata pesa zaidi, Grace niliyeingia Safari Club ni tofauti kabisa na niliyetoka humo siku hiyo,” alimalizia maneno hayo huku akiangua kicheko.

‘Tusker Fanya Kweli Uwini’ ni kampeni inayoendeshwa nchi nzima ambayo ilianza takribani wiki sita zilizopita na kujikita mikoa yote. Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Moshi ndiyo mikoa ya kwanza iliyoshuhudia uzinduzi wa aina yake na mpaka sasa promosheni hii imeonesha jinsi Watanzania wanavyokua mamilionea kwa kuwa washindi wa Milioni moja kila mmoja. Bado zimebaki Milioni 30 kushindaniwa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad