
Ufaransa yaelekea kurudia historia yake ya kunyakua mataji kila inapoandaa michuano fulani. Mfano waka 1998 walipoadaa michuano ya kombe la dunia, walifanikiwa kulichukuwa Kombe hilo, mwaka 2000 waliandaa michuano kama hii na kufanikiwa kulitwaa taji hilo, je watafanya hivyo tena mwaka huu siku ya jumapili Julai 10 2016 pale watakapopambana na Ureno kwenye mchezo wa fainali.
Ufaransa wametinga kwenye hatua hiyo baada ya kuwavurumisha Ujerumani kwa mabao 2-0 katika nusu fainali ya pili iliyokuwa ya kusisimua kwa muda wote wa mchezo.Walikuwa ni Ujerumani waliolisakama zaidi lango la Ufaransa lakini twaweza sema bahati haikuwa yao.

Ilikuwa dakika ya 45 mpira wa kona uliokuwa unatua kichwani kwa Patris Evra unazuiwa na mkono na Bastian Schweinsteiger na mwamuzi toka Italia Nicola Rizzoli anaamuru kupigwa mkwaju wa penati na hapo hapo anamzawadia Schweinsteiger kadi ya njano.
Antonie Griezmann anapiga penati kifundi akimpeleka kipa Neuer markiti upande wa kushoto na mpira unajaa kulia na kuiandikia timu yake bao la kuongoza.
Dakika ya 60 Ujerumani wanapata pigo baada ya beki wao mahiri Boateng kuumia na kulazimika kutoka nje na nafasi yake ikichukuliwa na Shkodran Mustafi.

Mnamo dakika ya 72 Paulo Pogba anapata mpira wingi ya kushoto anaucheza kwa staili ya Zidane kisha anapiga krosi safi ambayo kipa Wa Ujerumani Neuer anaipangua lakini mpira unamfikia Antonie Griezmann na kufunga bao pili. Hivyo mpaka mtanange huo unafikia tamati katika uwanja wa Stade Valendrome jijini Marseille, Ufaransa 2-Ujerumani 0.
Tusubiri jumapili nani kutwaa ubingwa UFARANSA au URENO?.
Tusubiri jumapili nani kutwaa ubingwa UFARANSA au URENO?.
No comments:
Post a Comment