Gari la Toyota aina ya Hilux ambalo lilizinduliwa mwishoni wa wiki jijini Dar es Salaam.
Meneja wa huduma kwa wateja na mahusiano wa Toyota Tanzania, Fatma Mussa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Uzinduzi wa Gari la Toyota la Furtuner na Hilux ambapo magari hayo yameboreshwa kwenye Injini pamoja na
matairi.
Toyota Tanzania imeboresha magari ya Hilux na Furtuner ambayo ni toleo la nane tangu kampuni hiyo kuanza kutengeneza magari.
Hayo yamesemwa na Meneja wa huduma kwa wateja na mahusiano wa Toyota Tanzania, Fatma Mussa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa magari hayo yanahimili mikikimikiki yote ya hali zote za barabara hasa barabara ambazo hazijaboreshwa.
Amesema kuwa Toyota Tanzania imeboresha magari hayo kwaajili kutumika na familia pamoja na kubeba mizigo au yanaweza kutumika katika starehe, kazini au shambani.
Fatma amesema kuwa magari hayo yameboreshwa kwenye Injini, imewekewa sehemu ya kupozea vinywaji au chakula (Friji)pamoja na sehemu ya Redio imewekewa kama Ipad, magari hayo yanamuweka dereva kuwa na utulivu wakati kuendesha magari.
Pia amesema kuwa magari hayo yameboreshwa matairi yake, sehemu ya kubeba mizigo, usalama wake pamoja na nguvu ya utendaji kazi wake.
No comments:
Post a Comment