Wananchi katika Kijiji cha Masinono wilayani Musoma wakitazama gari dogo la Wagonjwa likiingia katika Zahanati ya Kijiji hicho. Gari hilo limetolewa na Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Gari hizo Nne aina ya Suzuki Maruti alizikabidhi katika vijiji vya Masinono, Kurugee, Mugango na Nyakatende na kufikisha idadi ya gari Tano za wagonjwa alizozitoa katika Jimbo hilo.
Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini,
Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikabidhi leseni na funguo
ya gari ya wagonjwa (ambulance) kwa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo (katikati) na
anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naane
(kulia). Gari hizo Nne aina ya Suzuki Maruti alizikabidhi katika vijiji vya
Masinono, Kurugee, Mugango na Nyakatende na kufikisha idadi ya gari
Tano za wagonjwa alizozitoa katika Jimbo hilo.
Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini,
Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi wa Kijiji
cha Kurugee wilayani humo, kabla ya kuwakabidhi gari ndogo ya
wagonjwa aina ya Suzuku Maruti.
Wananchi wa Kijiji cha Kurugee wilayani Musoma wakimsikiliza
Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini,
Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani) kabla ya
kuwakabidhi gari ndogo ya wagonjwa aina ya Suzuku Maruti.
Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijijini,
Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo (wa Pili kulia) na Mkuu
wa wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naane (wa pili kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na na wananchi wa Kijiji cha
Kurugee wilayani humo, mara baada ya kuwakabidhi gari ndogo
ya wagonjwa iliyotolewa na Profesa Muhongo.
No comments:
Post a Comment