HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 19, 2016

KOZI YA MAKOCHA YA KUNDI "A" YAFUNGULIWA LEO NA MALINZI.



Makocha wakiwa katika picha ya pamoja na Raisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF jamali Malinzi.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Jamali Malinzi (katikati akizungumza wakati wa ufunguzi wa kozi za makocha leseni A wapatao 20 leo Jijini Dar es salaam.
Waamuzi wakiwa wanamsikiliza Raisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Jamali Malinzi wakati wa ufunguzi wa kozi ya ukocha ngazi ya CAF leseni A.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amezitaka timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuwa makini katika usajili wao wa makocha wa kigeni kuanzia msimu wa 2017/18 na ametoa wito huo wakati wa kufungua kozi ya makocha wa leseni A 20 niliyoifanyika Jijini Dar es salaam.

Amesema, timu hizo zinatakiwa kuhakiki wasifu wa makocha hao na kupeleka ripoti katika Shirikisho la soka Afrika (CAF) kabla ya kuwapa mikataba. Amevitaka vilabu  kabla ya kuingia nao mikataba wanatakiwa kuhakikisha kama wadhifa wao unaendana na vigezo zinavyohitajika Afrika ambapo daraja A ndilo daraja la juu kabisa na endapo CAF hawataridhishwa na viwango hivyo basi makocha hao hawataruhusiwa kufundisha mpira wala kukaa katika benchi la ufundi hapa nchini.

Malinzi amesema kuwa mbali ya walimu hao wa kigeni pia hakuna kocha yoyote mzawa atakayeinoa timu ya ligi kuu kama hana leseni ya daraja A kwani hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua kiwango cha soka la Tanzania na kuzidi kuku kuliko ilivyo sasa na makocha wa ligi daraja la kwanza watakaoruhusiwa kuzinoa timu ni wale wenye leseni B huku wenye leseni C wakinoa timu za daraja la pili.

"Tutahakikisha kuanzia msimu wa 2017/18 makocha wote watakazinoa timu za ligi kuu wanakuwa na daraja A pia makocha wa kigeni wataangaliwa zaidi ili kuondokana na vitendo vya udanganyifu", amesema Malinzi. Aidha aliwataka wanawake kujitokeza katika mafunzo hayo ili kusaidia harakati za kukuza soka la wanawake nchini.

Kwa upande wake Mkufunzi mwandamizi wa CAF, Sunday Kayuni alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kukubwa walimu kuwa na timu zenye wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa na endapo jambo hilo litafanikiwa basi ni wazi kuwa Tanzania ipatapa vijana wengi zaidi watakaocheza soka la kulipwa na kuzidi kupeperusha vema bendera ya nchi kupitia soka. "Ni imani yangu kuwa baada ya mafunzo haya ambayo ndiyo yanayotoa walimu wenye sifa za juu kabisa Afrika, Tanzania itaweza kuwa vizuri kwa upande wa soka na kuleta mabadiliko", alisema Kayuni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad