HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 18, 2016

JUMA ABDUL NDIE MWANASOKA BORA WA LIGI KUU TANZANIA BARA 2015/16

Beki wa kulia wa Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Juma Abdul, usiku huu ametangwazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2015/2016. 


Juma ameibuka kidedea na kutwaa Tuzo hiyo baada ya kuwagalagaza wapinzani wake beki wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shizza Kichuya na kujinyakulia kitita cha Sh. Milioni 9.2 

Aishi Salum Manula wa Azam FC ameshinda tuzo ya kipa Bora akiwamwanga Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga na Benno Kakolanya wa Prisons na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 huku mfungaji bora Amissi Tambwe wa Yanga akizawadiwa pia Sh. Milioni 5.7. 

Thabani Kamusoko ameibuka kidedea kwa kujinyakulia kitita cha Sh Milioni 5.7 baada ya kuwa mchezo bora wa kigeni na kuwagalagaza wenzake Donald Ngoma na kipa wa Simba, Vincent Agban. 

Aidha Kocha Mkuu wa Yanga Hans van der Pluijm, pia ameibuka mshindi wa Kocha Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 8, huku akiwaangusha Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar na Salum Mayanga wa Prisons. 

Mohamed Hussein 'Tshabalala' ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi akiwamwaga Farid Mussa wa Azam Fc na Shizza Kichuya wa Mtibwa Sugar na kuzawadiwa Sh. Milioni 4. 

Ibrahim Hajib wa Simba ameshinda tuzo ya Bao Bora la Msimu na kuzawadiwa Sh. Milioni 3 akimuangusha Tambwe wa Yanga, wakati timu ya Mtibwa Sugar ikiibuka kidedea baada ya kuzibwaga JKT Ruvu na Mgambo Shooting katika tuzo ya Timu yenye Nidhamu na kuzawadiwa Sh. Milioni 17.2. 

Ngole Mwangole ameshinda tuzo ya Refa Bora na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.7 baada ya kuwaangusha Anthony Kayombo na Rajab Mrope.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akimkabidhi Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Beki wa Yanga, Juma Abdul wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo za washindi wa Ligi Kuu iliyofanyika kwenye hoteli ya Double Tree By Hilton, usiku huu. 
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kuli) akimkabidhi mfano wa Hundi, yenye thamani ya Tsh M 5,740, Kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko. Kushoto ni mkewe Bongile Sibanda. 
Mohamed Mwameja (kushoto) akimkabidhi tuzo ya Kipa Bora wa Ligi Kuu, Aishi Manula. 
Wachezi wote waliotunukiwa Tuzowakiwa katika picha ya pamoja. 
1. Mchezaji Bora: Juma Abdul - YANGA 


2. Golikipa Bora: Aishi Manula - Azam FC 


3. Kocha Bora: Hans Van Pluijm - YANGA 

4. Mchezaji Bora Chipukizi: Mohammed Hussein -Simba 

5. Mchezaji Bora wa Kigeni: Thabani Kamusoko - YANGA 

6. Mfungaji Bora: Amiss Tambwe - YANGA 

7. Goli bora la Msimu lilifungwa na Ibrahim Ajib 

8. Timu yenye nidhamu: Mtibwa Sugar 

9. Mwamuzi Bora: Ngole Mwangole - MBEYA 

10. Zawadi za Washindi 

i) Mabingwa - YANGA Sh. Milioni 81.3 

ii) Washindi 2 - AZAM Sh. Milioni 40.6 
iii) Washindi 3 - SIMBA Sh. Milioni 29 
iv) Washindi 4 - TZ PRISONS Sh. Miloni 23.2 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad