Mussa Jumanne mtumbuizaji wa nyimbo za asili akiwa anatoa burudani katika eneo la Remsi, Mnazi Mmoja leo Jijini Dar es salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIPAJI kinachotembea, Kijana Mussa Jumanne mwenyeji wa Mkoa wa Mwanza ameamua kuja Jijini Dar es Salaam kujitafutia riziki kwa kutoa burudani kwa jamii mahali kokote wanapotaka huduma yake na amekuwa kivutio kwa watu wengi. Amekuwa akiiimba mashairi yenye ujumbe mbalimbali unaowagusa jamii na huo ndiyo mtaji wake katika kujiingizia kipato.
Jumanne akiwa na miaka 12 alianza kujihusisha na masuala ya kutumbuiza ila mwaka 2008 alijikita zaidi na akaamua kuweka fani yake mbele ikiwa ni moja ya ajira anayoitegemea kwa sasa kujiendeshea maisha yake na kupata kipato.
Akizungumza na Michuzi, Jumanne amesema kuwa ana mwezi mmoja toka aingie katika Jiji la Dar es Salaam, na ameweza kupata hamasa kubwa sana baada ya kuona watu wanapokea vizuri kazi yake na kuzidi kujituma zaidi kila siku. “ nimekuja Dar es salaam, namshukuru mungu nimefanikiwa kupata hamasa kutoka kwa jamii na kuzipenda kazi zangu kwani nachokiongelea hasa kweye mashairi yangu ni vitu vinavyotuzunguka na ukweli mtupu,”.
Amesema kuwa kama atapata sehemu maalumu atakayokuwa anafanyia kazi zake basi itakuwa vizuri sana kwani ana imani atazidi kuwa burudani watanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment