HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 19, 2016

BIA YA ASILI YA NZAGAMBA YAZINDUA PROMOSHENI YA AINA YAKE KANDA YA ZIWA

 Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo akionyesha kwa waandishi wa habari Bia hiyo ya Asili inayopatika maeneo ya Kanda ya Ziwa, wakati uzinduzi wa Promosheni yake itakayowawezesha wanywaji wa Bia hiyo kujishindia Ng'ombe kila wiki. Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 19, 2016 kwenye Kiwanda cha Nzagamba, Iloganzala Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo.
 Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo akionyesha moja ya maboksi yatakayotumika kwa washiriki wa Promosheni ya Bia hiyo ya asili ya Nzagamba itakayowawezesha wanywaji wake wa Kanda ya Ziwa kujishindia Ng'ombe kila wiki, wakati wa uzinduzi wa Promosheni hiyo, uliofanyika kwenye Kiwanda cha Nzagamba, Iloganzala Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo.
 Meneja Usambazaji wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Peter Mwambenja (kushoto) akielezea namna Promosheni hiyo itakavyofanyika na namna washindi watakavyopatikana. Wengine pichani ni Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo, Meneja Mauzo wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Fred Kazindogo pamoja na Meneja Usambazaji wa Bia ya Asili ya Nzagamba, James Makalla.
Meneja Masoko wa Bia ya Asili ya Nzagamba, Oscar Shelukindo akionyesha kwa mfano namna ya kushiriki Promosheni hiyo ya Nzagamba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad