Mara nyingi tumezoea kuangalia michezo fulani ikifanyika mahali fulani, mfano mwezi huu na mwezi uliopita tulishuhudia mashindano ya kabumbu ya Amerika ya kusini na yale ya Ulaya pia mashindano ya dunia ya riadha.
Lakini hivi sasa macho na masikio ya wapenda michezo duniani kote yataelekezwa jijini Rio de Jeneiro nchini Brazil ambako michezo ya OLIMPIKI itafanyika.
Michezo ya Olimpiki ni mashindano ya mkusanyiko wa michezo mbali mbali yanayofanyika pamoja (jiji moja) kila baada ya miaka minne.Baadhi ya michezo hiyo ni Mpera wa miguu,Mpira wa kikapu,Mpira wa magongo,Riadha, Ndondi,Judo,Kuogelea,Sarakasi nk.
Michezo ya mwaka huu itajumuisha Nchi zipatazo 206,Michezo takribani 42 itashindaniwa katika viwanja 37 kwa matukio 306.Michezo hii inatazamiwa kuanza Agust 5-21/2016.
Pia michezo hii huwa na kitu tofauti sana na michezo mingine,kitu hicho ni MWENGE wa Olimpiki,Mwenge huu huwashwa na kuzungushwa katika baadhi ya nchi kwenye mabara yote matano ya dunia ili kusisitiza umoja ma ushirikiano.Ukiangilia nembo ya Olimpiki utaona ina viduara vitano vilivyoungana,ikiwa na maana ya mabara matano ya dunia.
Usikose kujumuika nasi kesho ambapo tutakuletea utamu mwingine kuelekea michezo hii,kidokezo ni kuwa Nani mwanzilishi wa michezo hii,ilianzishwa lini na wapi?
No comments:
Post a Comment