HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 17, 2016

Wateja wa vodacom wafuatwa na Vodacom popote walipo.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mauzo na Usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh(kushoto)na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia(kulia)wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi wa kampeni maalum ya magari zaidi ya 40 yatakayozunguka nchi nzima,kwa ajili ya kuhamasisha na kutoa elimu ya huduma za kampuni hiyo ikiwemo kusajili laini za wateja kwa njia ya kieletroniki na kuwauzia wateja wake  simu halisi za gharama nafuu.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kushoto)akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya magari zaidi ya 40 yatakayozunguka nchi nzima,kwa ajili ya kuhamasisha na kutoa elimu ya huduma za kampuni hiyo ikiwemo kusajili laini za wateja kwa njia ya kieletroniki na kuwauzia wateja wake  simu halisi za gharama nafuu.

.Zaidi ya magari 40 yaanza safari ya kupeleka huduma mikoa yote nchini
.Gulio kubwa kufanyika Mlimani city kuanzia kesho mpaka jumapili 
Katika kutekeleza agizo la Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA)la kuzitaka kampuni za mawasiliano kutoa elimu kwa wateja wao kuhusiana na simu zisizokuwa na kiwango yaani simu feki,Vodacom Tanzania leo imezindua kampeni maalum ya uhamasishaji wa huduma zake mbalimbali ikiwemo kusajili laini za wateja kwa njia ya kieletronikali pia kuwauzia wateja simu halisi na za gharama nafuu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa bidhaa za Vodacom,Hassan Saleh amesema kuwa lengo ya kampeni hii itakayofanyika kwenye mikoa yote ya nchi,mijini na vijijini ni kutoa elimu na kutangaza  matumizi ya huduma mbalimbali za Vodacom pia kuwapelekea bidhaa bora za mawasiliano na za gharama nafuu.

“Kipindi hiki ambacho simu feki zinazimwa tumeona ni vema tuwafikie wananchi hususani wanaoishi maeneo ya vijijini na kuwauzia simu halisi na za gharama nafuu ili wasiachwe nje ya mawasiliano,pia tutasajili laini za wateja ambao walikuwa wanatumia simu bila usajili ili kuwaepusha kuangukia kwenye mkono wa sheria kwa kufanya hivyo vile vile tutawaelimisha jinsi ya kunufaika na huduma zetu mbalilmbali hususani huduma ya kukopa kwa kutumia simu ya mkononi ya M-Pawa bila kusahau huduma ya M-Pesa”.Alisema

Saleh alisema hii sio mara ya kwanza kampuni kuwafuata wateja imekuwa ikifanya hivyo mara kwa mara kwa kuwa inaamini kuwa wateja ndio namba moja katika biashara zote inazofanya “Kwetu wateja wetu ni wafalme,tanawapenda,tunawajali na kuwasikiliza ndio maana tumeona kuna umuhimu wa kuwafuata popote walipo na kuwaelimisha ni kwa jinsi gani watanufaika na huduma zetu na kuboresha maisha yao ikiwemo kuwapatia zawadi mbalimbali bila kusahau burudani zinazoenda sambamba na kampeni hii”.Alisema

Kuhusiana na huduma ya M-Pawa inaowawezesha wateja kujipatia mikopo kupitia simu zao za mkononi alisema huduma hii imeanza kupata mafanikio makubwa “"Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo wananchi wengi wamekuwa wakizidi kuelewa huduma hii mpya zaidi ya matarajio yetu na watu wengi wamefungua akaunti na wengine wanazidi kujiunga kila kukicha na wengi tayari wameanza kupata mikopo kupitia huduma hii.Mpaka sasa zaidi ya watanzania milioni moja wanatumia huduma hii”.Alisema.
Alisema teknolojia hii ya M-Pawa au “kibubu” ni mkombozi kwa wananchi wengi wa Tanzania ambao walikuwa hawajafungua  akaunti za benki “Kuna wananchi wengi wamekuwa na utaratibu wa kukaa na fedha nje ya mabenki,ambako hazileti riba zinawekwa kwenye magodoro,wengine kuzichimbia ardhini na darini,fedha hizi haziko salama ni bora kuziweka M-Pawa”anasema Saleh.

Aliwataka watanzania kuchangamkia fursa  hii kusajili laini za simu zao,kununua simu halisi na vifaa vingine vya mawasiliano bila kusahau kufika katika gulio kubwa na la aina yake hapo kesho katika makao makuu ya kampuni hiyo kuanzia saa 4 asubuhi.Alisisitiza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad