HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 10, 2016

MWASAPILI ACHEZA MECHI 28 ZA LIGI KUU.

BAADA ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara  2015/16  na Mbeya City fc kumaliza ikiwa kwenye nafasi ya 8 baada ya kuweka kibindoni jumla ya Pointi 35,  kufuatia  mabao  32  ya kufunga na kufungwa 34 kwenye michezo 30 ya msimu mzima.

Mlinzi Hassan Mwasapili (Kulia)ameweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi kikosini kuliko mchezaji yoyote kwa kucheza mechi 28 na kukosa 2  pia kuna rekodi kadhaa kutoka bechi la ufundi  zimetoka  na kati ya hizo baadhi  zinaonyesha kuwa, magolikipa watatu wa kikosi cha kwanza, Juma Kaseja, Haningtony Kalyesubula na Geoffrey Mwalyego  waliokuwa wakisimama langoni  kwa kupishana kwenye michezo tofauti wamewajibika kwa asilimia 33.33 katika ushindi, sare na hata kupoteza mchezo katika mechi zote 30 za msimu.

Katika rekodi hizo zinaonyesha,  Juma  Kaseja amecheza michezo 17 na kuruhusu kufungwa mabao 20, Haningtony Kalyesubula akicheza michezo 13 na kufungwa mabao 14 wakati Geoffrey Mwalyego yeye hakupata nafasi ya kucheza mchezo hata mmoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad