Unapozungumzia
Club bora jijini Dar es salaam huwezi kuiacha Club Triple 7 iliyopo
maeneo Kawe/Mikocheni ni sehemu ambayo mastaa wengi na watu mbali mbali
hupendelea kufika kwa ajili ya burudani nzuri ya muziki inayopatikana
hapo.
Siku
za jumatano huwa ni usiku wa Karaoke ambapo watu hufika hapo kwa ajili
ya kuimba nyimbo mbali mbali wazipendazo, lakini balaa zaidi huwa ni
siku za ijumaa na jumamosi ambapo huwa ni siku za Club kwa ajili ya watu
kula bata na kupata mziki mzuri.
Michael
Saduka si jina geni miongoni mwa masikio ya wasikilizaji wa radio hapa
nchini, ni mtangazaji aliyepitia kituo cha Times fm, Magic fm na E fm
ndie Dj wa Club Triple 7, nilishangaa kumuona Triple 7 kwa jinsi
anavyowarusha, watu mbali mbali ambao hufika hapo.
Nikapata
bahati ya kuzungumza na watu mbali mbali sababu ya kwanini hupenda
kufika Triple 7 licha ya Dar kuwa na Club mbali mbali wengi wamesema ni
huduma nzuri za vyakula na vinywaji ila funga kazi ni burudani ya Mziki
kutoka kwa Michael Saduka aka Dj Micklove
"
Huyu jamaa bwana anajua nini anachofanya ana selection nzuri ya music,
ana mix vizuri, anapiga ladha nzuri ambapo kweli una feel kuwa uko club,
Mimi nitaenda club zote lakini Triple 7 lazima nifike" Alisema mmoja wa
shabiki alikamatwa na Camera yetu.
Na
kwa upande wa Michael Saduka alipoulizwa anajisikiaje kuwapa burudani
wakazi wa jiji la Dar es salaam na kuchizika alisema "Mimi nahisi faraja
sana kwa maana muziki ninaujua kwa muda mrefu na ladha yangu ya muziki
iko tofauti sana na ma dj wengi na kuna wageni mbali mbali hutembelea
club yetu kutoka mataifa mbali mbali na nimeshapata mialiko mingi ya
kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuburudisha, am so proud to be at Triple
7, wategemee mambo makubwa" Alimalizia kusema Michael Saduka aka Dj
Micklove.
Hayo ndio mambo ya Triple 7, kama hujawahi kufika hebu fika weekend ukajionee burudani za uhakika.
Dj Michael Saduka akifanya yake ndani ya Club Triple 7, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Maua.
Show Love.








No comments:
Post a Comment