HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2016

TAKWIMU KUFANYA UTAFITI WA VIASHIRIA VYA UKIMWI NA MATOKEO TANZANIA 2016/2017

Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na masuala ya Afya – ICAP  kutoka chuo cha Colombia New youk, Dkt. Fernando Morales akizungumza mbele ya wadau wa Utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi wakati wa mkutano wa wadau ha oleo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa Akizungumza na wadau wa Utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi wakati wa mkutano wa wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tume ya Kudhiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Bibi. Fatma Mrisho Akizungumza na wadau wa Utafiti wa Viashiria na matokeo ya Ukimwi wakati wa mkutano wa wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa NBS jijini Dar Es Salaam leo.

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa katika utafiti wanaotarajia kuufanya wa viashiria vya Ukimwi na matokeo Tanzania 2016/2017 utakuwa na utofauti kutokana na kuanzia kwa vijana wa miaka 10 ili kuweza kuwa na takwimu sahihi hali ya ugonjwa huo.

Akizungumza na katika mkutano wa wadau wa utafiti viashiria vya Ukimwi na matokeo Tanzania 2016/2017, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk. Albina Chuwa amesema kuwa utafiti unahitaji ushirikiano na wananchi katika kuwezesha utafiti huo  kuleta matokeo chanya ya ugonjwa huo.

Amesema katika utafiti huo watapima kiwango cha C4 kwa watu wenye ugonjwa huo, ngono zembe katika katika kuweza kupata hali ya maambuzukizi mapya yako katika kiwango gani na umri upi umeweza kuathirika na ugonjwa huo.

Dk.Albina amesema utafiti huo unafanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau katika kupata hali halisi ya matokeo ya ukimwi ulivyofikia kwa sasa na kuweza kuchukua hatatu kutokana na matokeo hayo.

Nae Mwenyekiti wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), Amina Mrisho amesema  kufikia mwaka 2030 Tanzania inatakiwa kuwa na sifuri tatu kwa kuwa na unyanyapaa sifuri, maambukizi mapya sifuri na vifo vitokanavyo na ukimwi sifuri.

Amesema kuwa kutokana na nguvu za serikali kufikia mwaka 2030 watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi wawe wanaweza kujitamua hali zao kwa asilimia  90.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad