Na Bashir Yakub.
Mtu mmoja aliyeko Zurich alipiga simu akiuliza swali ambalo ni kichwa cha haya makala . Yeye yuko zurich lakini anataka kufunga ndoa na mwanamke aliyeko Tanzania bila kulazimika kurudi nchini. Anataka afunge ndoa akiwa hukohuko zurich na mwanamke akiwa Tanzania .
Alisema huko aliko jambo hilo linaruhusiwa kisheria ila wasiwasi wake ni kama hata Tanzania jambo hilo linaruhusiwa. Kabla ya kutizama jambo hilo kisheria upo umuhimu pia wa kutizama baadhi ya mambo kuhusu ndoa.
1.NINI MAANA YA NDOA.
Kwa mujibu wa kifungu cha 9( 1 ) cha sheria ya ndoa sura ya 29, ndoa imetafsiriwa kama muungano wa hiari kati ya mwanamke na mwanaume wenye lengo la kudumu maisha yao yote.
2. SHERIA INASEMAJE KUHUSU WAZAZI KUCHAGUA WACHUMBA.
Katika maana ya ndoa kuna neno hiari. Hili ni jambo la kwanza katika ndoa. Maana yake ni kuwa kusiwe na kulazimisha, ulaghai, udanganyifu n.k. Hata kurubuni kunakolenga kuondoa hiari ya mtu nako ni kulazimishwa. Pia wazazi kuwachagulia vijana wao wachumba na kuwashinikiza kuwaoa au kuolewa nao nako ni kuondoa hiari ya wahusika.
Si kosa mzazi kuona mchumba kwa ajili ya kijana wake isipokuwa ni kosa akitumia nafasi hiyo kulazimisha/kushinikiza kufungwa ndoa. Haya ni kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya ndoa.
No comments:
Post a Comment