Kamishina Jenerali wa Mageraza nchini John Carmir Minja afanya ziara ya kikazi Mkoani
Kagera yenye lengo la kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa wa Kagera pamoja
na kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo.
Akiwa Mkoani hapa Kamishna Jenerali Minja alifika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Mhe. John Mongella na kufanya naye mazungumzo kuhusu utendaji kazi na
ufanisi wa Jeshi la Magereza Mkoani hapa katika kuimarisha ulinzi na usalama.
Aidha katika mazungumzo hayo walizungumzia changamoto ya msongamano wa
Mahabusu katika Gereza la Wilaya ya Muleba ambalo hivi sasa linatumika kuhifadhi
Mahabusu wa Wilaya ya Muleba na Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambayo haina Gereza
la Wilaya.
Kamishna Jenerali wa Mageraza nchini John Carmir Minja pia alitembelea Mahakama
Kuu Kanda ya Bukoba na kufanya mazungumzo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo
Mhe. Sivangilwa Mwangesi juu ya namna ya kuongeza kasi ya usikilizwaji wa kesi
mbalimbali za watuhumiwa ili kuondoa msongamano Magerezani.
Vilevile Kamishna Jenerali Minja alitembelea Gereza la Wilaya la Bukoba na kuongea na
wafungwa na Mahabusu wa Gereza hilo pia na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la
zahanati ambalo lipo katika hatua za mwisho kukamilishwa ili liweze kutoa huduma za
afya kwa wafungwa na watumishi wa Jeshi hilo pamoja na wananchi wanaoishi jirani na
zahanati hiyo.
Kamishna Jenerali Minja yupo Mkoani Kagera kwa siku 7 kuanzia tarehe 10 hadi 16
Machi, 2016 ambapo lengo la ziara hiyo ni kutembelea na kukagua Magereza ya Mkoa
wa Kagera pamoja na kujionea miradi ya uzalishaji inayosimamiwa na jeshi hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja( wa pili kushoto) akikagua maeneo mbalimbali ya
Gereza Bukoba alipofanya ziara ya kikazi leo Machi 11, 2016 (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Kagera, SACP. Omari Mtiga (wa pili kulia) ni Mkuu wa Gereza Bukoba, ACP. Benizeth Bisibe.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella akiongea ofisini kwake na Kamishna Jenerali wa
Magereza John C. Minja na ujumbe wake kama inavyoonekana katika picha.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba Mhe. Sivangilwa Mwangesi Akisalimiana na
Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja alipomtembelea ofisini kwake.
Kamishna Jenerali wa Magereza John C. Minja (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kagera mara baada ya kutembelea Gereza la Wilaya
ya Bukoba (Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment