KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetuma salamu za pongezi kwa viongozi wapya wa Chama cha Wahariri Tanzania waliochaguliwa katika mkutano wao uliomalizika mwishoni mwa wiki.
Katika salama zake za pongezi Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema “Kwa niaba ya Vodacom nawapongeza viongozi wa Chama Cha Wahariri waliochaguliwa kuongoza Jukwaa la Wahariri nchini.
Aliongeza kuwa Vodacom itaendelea kufanya kazi kwa karibu na viongozi hao kwa kuwa inaamini kuwa vyombo vya habari ni njia kubwa inayotumika kwa mawasiliano kama zilivyo simu za mkononi na mawasiliano yakiwa mazuri katika jamii yoyote ile ni lazima ipate maendeleo kwa haraka.
Ferrao alitoa shukrani kwa uongozi uliomaliza muda wake kwa jinsi ulivyofanya kazi nzuri ya kukuza taaluma ya habari na kufanya kazi kwa ushirikiano na makampuni na taasisi mbalimbali.
Katika uchaguzi Bw.Theophil Makunga, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL) alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Mhariri Mtendaji wa Jamhuri, Deodatus Balile, amechaguliwa kuwa Makamu wake na Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena, ameendelea kuwa Katibu Mkuu wa jukwaa hilo.
No comments:
Post a Comment