Rais SAMIA SULUHU HASSAN ametoa kiasi cha Shilingi MILIONI HAMSINI kwa Taasisi ya Wanawake na SAMIA wa Mkoa wa Geita kwa ajili ya kuongeza mtaji wa zabuni ya kuwalisha watumishi zaidi ya MIA MOJA kwa siku wa Shirika la Madini la Taifa [STAMICO] ambao wanafanya kazi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita [GGML].
Mkuu wa Mkoa wa GEITA MARTINE SHIGELA amewakabidhi risiti ya kiasi cha fedha kilichowekwa katika akaunti ya Taasisi hiyo na Rais SAMIA na kuwataka kutumia fedha hizo kama ilivyokusudiwa ili kukuza mtaji na kupanua wigo wa kutoa huduma ya chakula katika makampuni mengine ya uchimbaji.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ADELINA KABAKAMA amemshukuru Rais SAMIA na wamesema mtaji huo utawainua na hawatakopa kwa sasa na wamesema Mkuu wa Mkoa MARTINE SHIGELA ndiye aliyewaunganisha na Shirika la Madini la Taifa [STAMICO] wamemshukuru na wamesema watajitahidi kujipambanua zaidi na kufanya shughuli za kuwalisha watumishi katika taasisi zingine na mashirika tofauti.
Rais SAMIA alitoa ahadi ya kiasi hicho cha fedha baada ya kutembelea katika banda la Taasisi ya Wanawake na Samia wakati wa kufunga maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini Mjini Geita na Taasisi hiyo walikuwa wanaonyesha matumizi ya nishati safi ya matumzi ya Mkaa unaoitwa RAFIKI BRIQUETTES.
No comments:
Post a Comment