
Mwandishi wetu Lindi
BARAZA la watoto mkoani Mkoani Lindi limefanya uchaguzi wa Viongozi wataliongoza kwa muda wa miaka miwili kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 baada ya viongozi waliokuwapo madarakani kumaliza muda wake kwa mujibu wa katiba.
Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa
Uliofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Save the Children International ambapo nafasi zilizogombewa ni pamoja na Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti,Katibu,Katibu Msaidizi Mtunza Hazina wajumbe kamati ya utendaji na kundi maalumu.
Msimamizi wa uchaguzi Afisa maendeleo mkoa Lindi, Anna Maro alimtangaza Aziza Ahmad kutoka wilaya Ruangwa kuwa Mwenyekiti baada ya kupata kura 9 na kuwashinda wapizani wake Salamu Mwinja kutokaWilaya Kilwa aliyepata kura 6 na siwafu mpende kutoka Lindi aliyepata kura 5 huku Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Shaibu Peleu kutoka wilaya Liwale badaa ya kupata kura 8 kati ya 18 zilizopigwa na kuwaacha wapizani wake wa wili wakigawanya kura sita sita kila moja.
Nafasi ya Katibu wa baraza hilo ilichukuliwa na Abdul Selema kutoka wilaya ya kilwa ambaye alipata kura 13 baada ya kumshinda mpizani wake Saidi Mohamedi kutoka Lindi mjini aliyepata kura 7 na Katibu Msaidizi alipata Swaumu Juma aliyepata kura 8 kati ya kura zote zilizopigwa.
Anna maro alimtangaza Sadamu Hamidu kutoka Kilwa kuwa Mhazini wa baraza hilo ambaye alipata kura 9 wakati Siwatu mpende kutoka Lindi Mjini alipata nafasi ya Mhazini Msaidizi kwa kupata kura 9
kwenye Uchaguzi huyo pia walichaguliwa wajumbe wawakilishi kundi maalumu wa baraza la Mkoa wa Lindi ambapo wajumbe ambapoArkama Kihaku kutoka wilaya ya Liwale alipata kura 17 na Nasoro isa kutoka Lindi Mjini alipata kura 2
Akizungumzia majukumu ya baraza la watoto Daudi Busweli Afisa Maendeleo ya jamii kutoka shirika lisilo la kiserikali la save the children ambalo linafadhili mabaraza ya watoto mkoa wa Lindi na shughuli za na kusimamia haki za watoto kwa kushirikiana na asasi za kijamii za Kingonet, Ropa na Lingonet alisema kuwa baraza la watoto linajukumu la kutambua haki za watoto na kuzisimamia haki hizo na kutafuta njia za kuondoa changamoto zinazosababisha watoto kutotendewa haki zao na jamii.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi huyo Mwenyekiti wa baraza hilo Aziza Ahmadi amesema kuwa baraza la watoto wilaya humo aliwavumilia wazazi, walezi na wananchi atakaye nyanyasa na kuvunja haki ya mtoto ya kupata elimu , Kulindwa kwa kumsababishia Mtoto wa kike hasa wanafunzi akwa kumpa ujauzito ,kushindwa kumpeleka shule kwa visingizio visivyo vya msingi.
Aidha Aziza Ahmadi amewashauri watoto hasa wa kike kuacha tamaa ambazo zinawaingiza kwenye matatizo yanayosababisha kupata mimba za utotoni ambazo zinaharibu malengo yao ,pia amewataka wazazi kuwalinda watoto wao ili wasiingie kwenye vishawishi hasa wanapokuwa shuleni kwani vishawishi hivyo ndivyo vinapelekea wao kushindwa kuendelea na masomo,
Aziza amevitaja vishawishi hivyo kuwa ni pamoja na simu za Mkononi ambazo zinajenga uhusiano wa karibu wa wanaume au wanawake wenye tabia za kuwaingiza watoto kwenye matendo yanayokwenda kinyume na haki za watoto na maadili
Aidha ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa baraza la watoto ili liweze kufanya kazi yake bila vikwazo kwa maendeleo ya watoto ambao ni taifa tegemewa la kesho.
No comments:
Post a Comment