HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 26, 2016

AIRTEL FURSA YAINUA KIKUNDI CHA VIJANA WAJASIRIAMALI MJINI LINDI.

 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kushoto), akiwapongeza kikundi cha vijana watano wajasiriamali  kijulikanacho kwa jina la Sauti ya Jamii baada ya kuwakabidhi msaada wa Zizi jipya la mbuzi, mbuzi 44 na vitendea kazi  kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ mjini Lindi katika mtaa wa Kariakoo. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Afisa maendeleo ya vijana mkoa wa lindi Sauda Mponjoli akifuatiwa na Afisa Utamaduni Mkoa, Makalaghe Shekhalaghe.
 Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa pili kushoto), akiwapongeza kikundi cha vijana watano wajasiriamali  kijulikanacho kwa jina la Sauti ya Jamii baada ya kuwakabidhi msaada wa Zizi jipya la mbuzi, mbuzi 44 na vitendea kazi  kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’ mjini Lindi katika mtaa wa Kariakoo. Wanaoshuhudia (kutoka kulia) ni Afisa maendeleo ya vijana mkoa wa lindi Sauda Mponjoli akifuatiwa na Afisa Utamaduni Mkoa, Makalaghe Shekhalaghe.
Meneja wa Huduma za jamii Kampuni ya Airtel Tanzania,Bi Hawa Bayumi (kati) akitoa elimu Kwa Afisa Utamaduni Mkoa,Makalaghe Shekhalaghe (kulia) pamoja na Afisa Vijana mkoa Lindi Bi Sauda Mponjoli (wa pili kulia Jinsi Airtel inavyotoa Fursa kwa Vijana Kupitia Airtel Fursa wakishuhudiwa na vijana wa kikundi cha Sauti ya Jamii waliowezeshwa na mradi huo wa Airtel Fursa kwa kupatiwa  Zizi jipya la mbuzi, mbuzi 44 na vitendea kazi vyenye dhamani ya shs milioni 10.

 WAFANYAKAZI wa kampuni ya simu za mkoni ya Airtel mkoani Lindi wamejumuika katika mradi wa kijamii wa  kampuni yao wa Airtel FURSA kwa kuwawezesha vijana wajasiriamali wa kikundi cha sauti ya jamii mkoani humo kwa kuwainua kibiashara na kuwajengea banda la ufugaji wa mbuzi la kisasa na kuwaongezea mbuzi 44 pamoja na vitendea kazi kama vile majembe na rato kwa ajili ya kuanza kilimo.

Vijana hao wapatao watano waliamua kuungana kwa pamoja baada ya kupata mafunzo kwenye mradi wa Kijana Jiajiri uliokuwa unaendeshwa na shirika la Restless Development ambao ulilenga vijana walio nje ya shule; kuwajengea uwezo ili waweze kujiajiri wenyewe na kupunguza ukosefu wa ajira nchini.

Kikundi cha Sauti ya Jamii kimesajiliwa na halmashauri, na kiliomba ardhi serikali za mitaa kwa ajili ya kilimo na kikapewa ekari 50, hivyo ukosefu wa mtaji ndio uliwakwamisha kuanza shughuli za  kilimo.

Akiongea wakati wa ujenzi wa banda hilo la kisasa la mbuzi  kiongozi wa msafara wa ziara hiyo na meneja mauzo kanda ya Lindi Edmund Lasway  alisema “Airtel tunayofuraha kuona tunaweza kusaidia vijana wenye moyo wa kujiendeleza kama hawa. Kabla ya hapa wamekuwa na mbuzi wapatao kumi na nne ambapo hawakuweza kuwapatia faidi ya kutosha, lakini kutokana na ongezeko hili la mbuzi na vitendea kazi kwa ajili ya kuinua biashara yao  ili waweze kutimiza malengo yao mengine makubwa waliyojiwekea  kama vile ya ukulim” .

Ni matumaini yetu kuwa fursa hii itawawezesha kufika mbali kibiashara na kutanua wigo wa biashara yao kwa kupata masoko na kuuza mifugo na kulima mazao yao katika ubora zaidi . Tunatoa wito kwa vijana wengine  kujitokeza na kutokukata tamaa ya maisha na kuchangamkia fursa kama hizi pale zinapojitokeza.

Kwa upande wake mwakilisha wa kikundi cha Sauti ya jamii, Shabani Kikotokeki, alisema “tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha kuinua biashara yetu na kutupa nguvu zaidi ya kujiendeleza kibiashara na hata kuwatia moyo vijana wenzetu wanaotuzunguka. Tunategemea kuinua kipato chetu na hata familia zetu  hivyo tunawahimiza vijana wengine hapa nchini kutokukata tamaa ya maisha na kuchangamkia fursa hizi zinapojitokeza.





Airtel kupitia huduma zake za jamiii imeweza kuwafikia vijana zaidi ya 20 kwa kuwapatia vitendea kazi katika msimu huu wa pili wa Airtel FURSA na kwa upande wa mafunzu ya biashara ya ujasiriamali imewafaidisha vijana wapatao 1000 katika  msimu huu wa pili wa  Airtel FURSA ambapo lengo ni  kufikia vijana wengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad