Matukio ya Wizi wa Maji yamekuwa yakikithiri kila kukicha katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam licha ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Mamlaka husika za kisheria pindi mtu au kikundi cha watu kinapobainika kufanya ubadhirifu huo.
Shirika la majisafi na Majitaka Dar es salaam(DAWASCO), imewakamata raia 2 wa china ambao wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume na taratibu katika eneo la Buguruni Jijini Dar es salaam, katika godauni moja inayomilikiwa na kampuni ya ALLIED TRANSPORT, jengo ambalo wachina hao wamepanga huku wakiendesha shughuli zao za utengenezaji wa mabati.
Kampuni hiyo ya wachina inayojishughulisha na utengenezaji wa mabati imebainika kujiunganishia huduma hiyo na Meneja wa Dawasco Wilaya ya Ilala Mhandisi Ramadhani Mtindasi wakati wa msako mkali ulioanza katika wilaya yake ya kuwabaini wahujumu miundo mbinu ya Maji na wezi wa Maji.
Mhandisi Mtindasi amesema kuwa matukio ya Wizi wa Maji kwa wilaya ya Ilala yamekidhiri sana na yanapelekea adhari kubwa sio tu kwa shirika bali hata kwa watumiaji wa Maji waliopo eneo la Ilala kutokana na Maji mengi kuishia mikononi mwa wachache hivyo kupelekea uhaba na kero ya Maji kwa maeneo yenye stahili ya Maji.
“tunasikitishwa na namna ambavyo wizi huu unaendelea kushika kasi katika wilaya yetu, hiki kiwanda cha Mabati kinajiendesha kwa faida ambayo inatosheleza kabisa kuunganisha Maji kwa taratibu husika na kuweza kulipa bili yao ya Kila mwezi” alisema Mhandisi Mtindasi.
Pia, alisema hasara iliyosababishwa na wizi huo wa kiwanda cha Bati imeigarimu DAWASCO hasara ya zaidi ya Tsh Milion 6 Na hivyo wamepeleka madai husika kwa mwenye kiwanda ili waweze kulipa fidia hiyo kwa kosa la kujiunganishia Maji kinyume cha sheria.
“utaratibu uliowekwa na DAWASCO huwa tukikamata mtu aliyejiunganishia Maji kinyume na taratibu huwa tunafanya hesabu ya miezi 24 nyuma yaan miaka miwili na kumpa gharama zake, ndio maana gharama iliyokuja kwa upande wa kiwanda hicho ni Tsh milioni 6 na zaidi ” aliongeza Mtindasi.
Kwa upande wa watuhumiwa hao raia wa Kichina ambaye alijitambulisha kama msimamizi wa shughuli za kiwanda hicho cha Bati ,Bi Yun Fei alisema waliunganisha Maji hayo kinyume na utaratibu kwa kutumia vishoka ambao walimtapeli kuwa wangeweza kumuunganishia huduma hiyo bila kukamatwa na DAWASCO.
Akiongea lugha ya Kiswahili kwa shida aliongeza kuwa wao hawajui lolote ila walitapeliwa kupewa huduma hiyo na mmoja wa vijana aliyeletwa ofisin kwao na kasha kuunganishwa huduma hiyo ya Maji huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu.

No comments:
Post a Comment