


KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imeendelea na harakati zake za kimasoko kutambulisha intaneti yake yenye kasi na bora zaidi ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam ili kuwafikia watanzania walio wengi zaidi.
Tangu kuzinduliwa kwa Huduma hii mwishoni mwa mwezi wa Desemba, 2015, wateja wengi wamefurahishwa na huduma hii kutokana na ubora wa intaneti, gharama nafuu ambayo inakidhi mahitaji yao. “Kweli nimeridhishwa na huduma zao, kwa sasa natumia kifurushi cha Oneconnect ambacho napata huduma za data ya 4G na ADSL (fixed modem), hii inanisaidia nikiwa nyumbani na nikirudi nyumbani naendelea kupata huduma kama kawaida kwa bei moja” alisema mteja, Boazi Kaaya.
Pichani juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE kwa wateja anuai.
Pichani juu ni baadhi ya akinadada wawakilishi wa Kampuni ya TTCL wakizungumza na wateja barabarani jijini Dar es Salaam kuitambulisha huduma ya 4G-LTE kwa wateja anuai.





“Ukienda kwenye ofisi zetu na vituo vya huduma kwa wateja utapata huduma hiyo mara moja” amesema Beda Kinunda Hivi karibu TTCL ilizindua huduma za 4G LTE kwa jiji la Dar es salaam ambayo inapatikana katika maeneo Posta(City Centre), Kariakoo, Upanga, Magomeni, Kijitonyama, Oysterbay, Ubungo, Mbezi, University of Dar es salaam, Pugu Road, Airport, Quality Centre, Kisutu, Mwananyamala, Kurasani na Tabata. Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inatekeleza mkakati kabambe wa mabadiliko ya kibiashara wenye lengo mahsusi la kuleta mageuzi makubwa katika biashara ya mawasiliano simu na Data nchini.
Baadhi ya mabango yakiwa yamewekwa na Kamapuni ya TTCL katika maeneo ya makutano ya barabara Mwenge na Kawe jijini Dar es Salaam kuitambulisha bidhaa ya 4G-LTE kwa wateja wa jiji la Dar es salaam.

No comments:
Post a Comment