HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 12, 2016

SERIKALI yakusudia kuanza kuzalisha drip za maji za IV katika hospitali zake zote kubwa nchini

SERIKALI inakusudia kuanza kuzalisha drip za maji za IV (Intravenous Fluids) katika hospitali zake zote kubwa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea mtambo wa kutengenezea drip hizo za majimaji katika hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho, Mkoani Ruvuma.

Amesema haoni kwa nini hospitali hizo ziendelee kuagiza wakati uwezo na watalamu wa kufanya hivyo upo hapa hapa nchini.

Drip hizo zina manufaa makubwa kwa wagonjwa ikiwemo kuongeza maji kwa wagonjwa waliopungukiwa na maji mwilini na vilevile inatumika kwa ajili ya kutolea baadhi ya dawa ambapo huchanganywa.

Vilevile hutumika wakati wa huduma za upasuaji.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiongea na Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Peramiho, Dr. Venance Mushi alipotembelea hospitali hiyo leo asubuhi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisalimiana na Padre Lucius wa Hospitali ya Peramiho, mkoani Ruvuma.
Baadhi ya wanachama wa NHIF wakiwa sehemu ya mapokezi tayari kupata huduma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad