HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 23, 2016

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ASALIMIA WANANCHI JIJINI ARUSHA AKIWA NJIANI KUELEKEA MONDULI KIKAZI

Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine jana kafunga zoezi la Onesha Uwezo Medani na  leo  anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani Monduli.
Baadhi ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema jana  asubuhi.
Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO na KISONGO


 Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani Arusha
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati wa ufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo Medan.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la Ufungaji.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi (kulia) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis Mwamunyange (wa pili kulia).
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange  na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad