Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inatarajia kupeleka kesi 36 mahakamani kwa tuhuma za kushiriki katika vitendo vya rushwa.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamishina Valentino Mlowola kuwa atafanya kazi hiyo ikiwa ni dhamira ya Rais kuhakikisha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi yanashughulikiwa bila kumuonea huruma
Amesema taasisi zitakazopelekwa Mahakamani ni Lake Oil katika kesi ya ukwepaji kodi katika shauri linalohusu udanganyifu na ukwepaji kodi.
Kamishina, Mlowola amesema kesi hiyo Lake Oil ilidanganya kwamba lita za mafuta ya petrol 17,461,111,.54 zimesafirishwa kwenda nchini Congo kupitia Zambia na kuisababishia hasara serikali sh.bilioni 8.5 wakati wa mafuta hayo yaliuzwa katika soko la ndani.
Kesi nyingine ni malipo ya dola za Marekani 6,000,000 ambazo kampuni ya EGMA kwa madai kuwa malipo ya kampuni hiyo kwa kusaidia Tanzania kupata mkopo dola za Kimarekani bilioni mia sita na kutakatishwa na watumishi wa umma wasio waaminifu kwa kushirikiana na baadhi ya watu wa sekta binafsiwakifahamu kuwa fedha hizo wamezipata kwa njia haramu.
Kamishina Mlowola amesema baadhi ya watumishi wataofikishwa mahakamani ni Shirika la Hodhi la Reli Nchini (RAHCO) kwa kukiuka kanuni na taratibu za kuwapata wazabuni wenye ujenzi wa wa reli ya Kisasa ya Kimataifa.
Katika Mlolongo kesi ni pamoja na kesi ya mabehewa ya Kokoto ya Shirika la Reli Nchini katika ukiukwaji wa manunuzi wa mabehewa 25 ya kokoto.
Aidha amesema kuwa kesi zote zimekamilika kwa uchunguzi na wameshapeleka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini kuomba kibali cha kuwafikisha mahakamani kwa wale wote waliobainika kujihusisha na matendo ya rushwa na ukiukwaji wa sharia ,taratibu na Kanuni za manunuzi wa Umma.
Amesema watumishi wa wa umma wafanye kazi kwa sheria na maadili kwani Takukuru haitawavumilia watu wataohusika na rushwa katika mazingira ya kazi.
Kamishina Mlowola amesema kuwa kazi alionayo ni kwenda sambamba na Rais Magufuli dhidi ya mapambano ya rushwa na ufisadi kwenda kwa vitendo bila ya kumuonea mtu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini jijini Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mikakati mbalimbali ya taasisi hiyo ya kupambana na rushwa nchini hasa kwa watendaji wa Umma na kesi zinazochunguzwa ili watuhumiwa wafikishwe mahakama wakati wowote baada ya kukamilika kwa uchunguzi wake.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Kulia ni John David wa Gazeti la Majira.
Mwendeshaji wa Mtandao wa Fullshangwe, John Bukuku (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment