HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 12, 2015

KAMPUNI 15 ZASHINDWA KULIPA KODI ZA KONTENA 329 ZILIZOTOROSHWA KATIKA BANDARI KAVU YA AZAM

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

KAMPUNI 15 zimeshindwa kulipa kodi za kontena zilizotoroshwa katika bandari kavu ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa na kodi iliyokuwa imekwepwa kwa kampuni 43 ni zaidi ya Sh. Bilioni 12.

Kodi iliyolipwa ya Kontena 329 hadi jana ambayo ndio ilikuwa ulipaji wa hiari kwa ndani ya siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ni zaidi ya sh. bilioni 10 pekee.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamisha Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo zinatakiwa kulipa kodi hiyo kwani ulipaji wa hiari wa siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli umeisha jana  hivyo hatua zitachukuliwa kuhakikisha wanalipa kodi hiyo ya Watanzania.

Mpango amesema kuwa kampuni 13 tu ndio zimeweza kumaliza kodi  yote iliyokuwa imekadiriwa na TRA kwenye Kontena 329 zilizotoroshwa katika Bandari Kavu ya Azam (ICD).
Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua za ulipaji wa kodi iliyokwepwa katoka katika kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam,leo jijini Dar es Salaam.

Amesema kampuni 15 zimelipa sehemu ya kodi na wanaendelea kuwadai licha ya kuisha kwa siku saba hivyo wanawajibu kulipa kodi iliyobaki katika Akaunti ya TRA iliyofunguliwa Benki Kuu (BoT) yenye namba 9921169 785.

Mpango amesema  kuwa wafanyabiashara ambao wameshindwa kulipa katika hicho hatua zitachukuliwa na wasubiri cha moto.

Aidha amesema mmiliki wa Bandari Kavu ya Azam ya Said Salim Bakhresa anakumbushwa kulipa kodi yote ambayo bado anadaiwa kwa mujibu wa nafasi yake kutokana na dhamana ya leseni ya Bandari Kavu (ICD).

Amesema watumishi 36 wa TRA wanatuhumiwa kushiriki katika upotevu wa kodi kutokana na kontena 329  kuondoshwa bandarini kinyume cha taratibu za forodha na hivyo kusababisha serikali ikose mapato.

Mpango amesema kuwa TRA inawaomba wananchi taarifa juu mali za kifisadi na mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo.

Amewataka watumishi kuwasilisha tamko za mali wanazomiliki pamoja na fedha zilizo katika benki na mwisho wa kufanuya hivyo ni Desemba 15 mwaka huu..
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa kwa Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad