Bwn. Daniel Korona akisherehesha hafla fupi
ya kumuaga Balozi wa Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake Mhe. Amina
Salum Ali iliyoandaliwa na Jumuiya ya Diaspora kutoka Afrika wanaoishi
Montgomery county iliyofanyika siku ya Jumatano Sept 2, 2015 Silver
Spring, Maryland.
Kulia
ni mwongozaji maswali Bi. Soffie Ceesay ambaye ni mwanachama
mwanzilishi wa Montgomery County's African Affairs Advisory Group na
African Immigrant Caucus akimuuliza Mhe. Amina Salum Ali maswali
mbalimbali likiwemo nini anajivunia kwenye uongozi wake kama Balozi wa
kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani. Balozi Amina Salum Ali
alieleza ni ushirikiano wa nyanja mbalimbali mabalozi
nchi za Afrika zimenufaika na kupata mafanikio na uhusiano wa AU na
Marekani kwa kuwezesha kupata Balozi wao nchini Marekani na kikubwa
kabisa katika historia ya AU na yeye kama Balozi kuwezesha Rais Barack
Obama kwa mara ya kwanza katika historia kama Rais wa Marekani kuhutubia
Umoja huo.
Isiah Leggett ambaye ni Montgomery County Executive akimtunukia cheti Mhe. Balozi Amina Salum Ali
Balozi
Amina Salum Ali akitoa shukurani zake ambapo leo anaondoka kurudi
Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa
Afrika nchini Marekani kazi aliyoifanya tangia 2006.
Wageni waalikwa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment