WIKI ya nenda kwa usalama ni muhimu katika jitihada za kuboresha masuala ya
usalama barabarani ikiwa ni jambo lililo na kipaumbele katika ajenda za
kitaifa nchini Tanzania.
Wiki hii inatoa misingi ya kufanya kazi
kuelekea katika kufikia maono na matarajio ya mazingira salama na
kuboresha usalama barabarani.
Hivi karibuni mwenyekiti wa tume ya
usalama barabarani bwana Elifadhili Mgonja wakati akiongea na waandishi
wa habari katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama jijini Dar es
salaam yaliyo fanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwa mwaka 2015/16
alisema kuwa ajali za barabarani zimekuwa ni chanzo kikuu cha kupoteza
maisha na mali nchini Tanzania. Ajali hizi zimekuwa chanzo kikubwa cha
vifo na ulemavu ambao unasababisha kudumaa kwa maendeleo ya watu
kiuchumi na kuathili uchumi wa taifa kwa ujumla.
Upigaji
vita ajali za barabarani nchini limekuwa ni suala linalopewa kipaumbele
kwani ajali mbaya zimekuwa zikiendelea kutokea. Pamoja na sababu
nyingine, miundombinu mibovu, uchovu kwa madereva, uchakavu wa magari
kama kukosa breki kutokana na kutokuwa na matengenezo imekuwa ni chanzo
kikuu cha ajali mbaya nchini Tanzania.
Kwa
nyakati tofauti, akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni katika
ofisi za kampuni ya Diamond Motors Ltd (Hansa) iliyopo katika barabara
ya Nyerere, meneja mkuu (masoko) wa kampuni hiyo Ndugu Laurian Martin
aliwaasa watanzania kuweka kipaumbele katika “usalama kwanza”.
Aliongeza kwa kusema kuwa utumiaji wa magari yaliyoboreshwa katika
teknolojia ambayo kwa sasa yanapatikana katika soko la Tanzania kama
vile malori ya Fuso FZ an Fuso FJ yanatoa nafasi kubwa ya kupunguza
ajali za barabarani.
Martin aliongeza kusema kuwa “Malori ya Fuso FZ
yanauwezo mkubwa wa breki zenye ukubwa, upana na unene unaolingana
katika magurudumu ya mbele na ya nyuma, pia ina kifaa cha kujazia upepo
pamoja na matanki ya kuhifadhia yanayokuhakikishia usalama wa hali ya
juu katika miundombinu ya Tanzania na masafa marefu.
Malori haya pia
yana vifaa maalumu sehemu ya mbele kwaajili ya kuzuia gari isianguke na
kubilingika kirahisi ikiwa ni pamoja na mfumo wa matairi mpana
unaoongeza ustahimilivu. Hivi ni vipengere muhimu sana hasa katika
barabara mbovu na uendeshaji wa hali iliyokithili.
Bwana
Martin aliendelea kwa kusema kuwa uchovu kwa madereva pia unachangia
katika ajali za barabarani hasa katika uendeshaji wa masafa marefu.
Malori ya Fuso FZ kutoka Diamond Motors yana kibini iliyo ninginizwa
vizuri katika mihimili yake ambayo inasaidia kupunguza mtikisiko hasa
katika matuta ya barabarani, haipati joto wala makerele kutoka kwenye
injini, pia ina kiti ambacho kina rekebishika pamoja na usukani unaoweza
kurekebishika. Vipengele hivi vinampatia dereva unafuu wa kuendesha
ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezekano wa kusababisha ajali.
Usalama
barabarani ni muhimu sana kwa watanzania na hii inadhihirishwa kwa
uwepo wa wiki hii ya nenda kwa usalama nchini Tanzania ikiwa ni nia
thabiti ya kupunguza ajali za barabarani. Muunganika wa sababu mbali
mbali za kiusalama ukizingatiwa inaweza kupunguza ajali za barabarani.
Usimamizi wa usalama barabarani kutoka kwa washikadau wa sekta hii,
mafunzo muafaka kwa madereva ikiwa ni pamoja na utumiaji wa magari
yaliyoboreshwa kwa ubora kama vile Fuso FZ na Fuso FJ ambayo hayahitaji
matengenezo ya mara kwa mara na yametengenezwa kwa teknolojia
iliyoboreshwa katika kumpunguzia dereva uchovu na ubora wa kuhimili
miundombinu ya Tanzania inaweza kuchangia katika uboreshaj wa usalama
barabarani.
Kuhusu Diamond Motors Limited (Hansa Group)
Diamond
Motors Limited imekuwa wasambazaji pekee wa malori ya Fuso nchini kwa
zaidi ya miaka 30. DML imeweka rekodi katika secta ya magari, kwa
kufanya kazi kwa ushirikaino na makampuni ya magari yenye ubora wa hali
ya juu zaidi duniani. Ushirika wao imara na makampuni yanayoongoza
duniani kama vile magari ya abiria ya Mitsubishi kutoka Japani, matairi
ya Yokohama kutoka Japani, MTU na ZF kutoka Ujerumani yameleta umaarufu
na kutoa uwanja mpana wa wateja kutoka sehemu mbali mbali za ukanda huu.


No comments:
Post a Comment