HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 15, 2015

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA MAPOKEZI YA LOWASSA JIJINI ARUSHA LEO

Umati wa Wakazi wa mji wa Tengeru, ukiwa umefurika kwa wingi barabarani kumlaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa alipopita eneo hilo, wakati akielekea Jijini Arusha kwenye Mkutano wa hadhara wa kutambulishwa kwa Mgombea huyo kwa wananchi wa Arusha,uliofanyika kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwa wamesimama pamoja na wananchi wa Jiji la Arusha walifurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015, wakati wa kuimba wimbo wa Taifa.
Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kamandolu, leo Agosti 15, 2015, kulikofanyika Mkutano wa kumtambulisha.
Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na maelfu ya wananchi wa Jiji la Arusha, wakati akimtambulisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, wakati wa Mkutano wa kutafuta udhamini wa Tume ya Uchaguzi na kutambulishwa kwa Mgombea huyo na Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kimandolu, leo Agosti 15, 2015.
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha. 
 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakifanyia Ibada ya kimila na Wazee (Malaigwanani) ya Kimasai, wakati wa Mkutano wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.

 Mke wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia wananchi wa jiji la Arusha.










































No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad