HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 16, 2015

WATANZANIA WAISHIO BOTSWANA KUANZA KUFAIDIKA NA MFUKO WA GEPF KUPITIA MPANGO WA ‘GEPF DIASPORA SCHEME’ (GDS)

Ujumbe wa Mfuko wa GEPF nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Watanzania waishio nchini Botswana wakiongozwa na Meneja Mahusiano wa Benki ya FNB Botswana, Bibi Patricia Mpelega (wa pili kushoto) wakati wakielekea kwenye tawi (Branch) la benki hiyo kwaajili ya uzinduzi wa akaunti maalum ya kuwasilisha michango kwa Watanzania wainshio nchini humo, kwa kujiwekea akiba zao za baadae.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko kutoka Mfuko wa GEPF, Aloyce Ntukamazina (wa tatu kulia) akimpa maelezo mafupi juu ya mpango huo wa GDS Meneja Mahusiano wa Benki ya FNB Botswana, Patricia Mpelega, muda mfupi kabla ya kuzindua akaunti maalum.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa watanzania waishio Botswana, Nieman Kissasi (kulia) na Meneja wa Mkoa wa Ilala Bw Jafari Meraji .
Bi Patricia Mpelega akimpongeza Mwenyekiti wa watanzania waishio Botswana, Nieman Kissasi baada ya kukamilisha zoezi la ufunguzi rasmi wa akaunti ya Diaspora Botswana
Mwenyekiti wa Watanzania waishio Botswana Bw Nieman Kissasi akikamilisha utaratibu wa kuwasilisha michango yake kama ishara ya uzinduzi rasmi wa akaunti hiyo kulia kwake ni Meneja wa Mkoa wa Ilala Bw Jafari Meraji
Mwenyekiti wa Watanzania waishio Botswana Bw Nieman Kissasi akiwasilisha mchango wake katika akaunti maalum ya Diaspora kwa ajili ya akiba yake kupitia Mfuko wa GEPF
Ujumbe kutoka Mfuko wa GEPF pamoja na Mwenyekiti wa Watanzania waishio Botswana wakiagana na Meneja wa Tawi la FNB Botswana

1 comment:

  1. These are highly welcome developments. I sincerely hope that many Tanzanians living in Botswana will benefit from GEPF

    ReplyDelete

Post Bottom Ad