Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana jijini Johannesburg mbali na mambo mengine nilihimiza sana ushirikiano baina yetu kwani wahalifu mtandao wameendelea kua mbele yetu kutokana na ushirikiano mkubwa waliokua nao. Ushirikiano unao mabatana na kusambaza vitendea uhalifu mtandao bure auu kwa gharama nafuu mitandaoni.
Baada ya kulizungumza hili laushirikiano wazungumzaji wengine wote walionekana kuniunga mkono na hatimae kuonekana ni swala muhimu lakufanyiwa kazi mapema. Nafarijika kuona Uingereza tayari mukuu wake wa CERT ametilia mkazo kauli hii (Ya ushirikiano) kupitia kikao kilicho malizika London ambapo taarifa kamili kuhusiana na hili inaweza kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA”
Aidha, Marekani na Israel baada ya kutia saini makubaliano ya kuboresha ushirikiano katika maswala ya usalama mitandao paliambatana na kuhimiza mataifa mengine kuona umuhimu wa kushirikiana katika vita hii ya uhalifu mtandao.

No comments:
Post a Comment