Wakazi
wa Mkoa wa Geita maeneo ya Buseresere na Katoro wapo katika hatari
kubwa ya maisha yao kutokana na usafiri wanaoutumia kutoka eneo moja
kwenda jingine.
Mwakilishi wa kikundi cha usalama barabarani Fungo Agustus ametutumia Tukio hili ambalo ni hatari kwa abiria mkoani Geita.
Gari
ndogo aina ya Pro Box zimeingia kwa wingi mkoani Geita na kutumika
kubebea abiria katika mazingira ambayo si salama na ni hatarishi kwa
abiria hao.
Abiria
wamekuwa wakipakiwa kwenye mabuti ya kuwekea mizigo tena kwa msongamano
mkubwa.Zifutazo chini ni picha za kinachoendelea kwenye usafirishaji
eneo la Buseresere.
Abiria wakiwa wamekusanywa kwenye buti eneo la kubebea mizigo huku wakiwa sambaba na watoto wadogo.
Aina nyingine ya Gari ndogo inayotumika kubebea abiria
Mizigo na Watoto wakiwa wamekusanywa pamoja na mizigo nyuma ya Gari hiyo
No comments:
Post a Comment