Daktari Bingwa wa Watoto na magonjwa ya figo, Jacquline Shoo akitoa
maelezo kwa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika
kikao cha kuhitimisha (Exit Meeting) la huduma za madaktari Bingwa hapa nchini.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, akishuukuru
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili katika kikao cha kuhitimisha zoezi.
Mkurugenzi
wa Huduma za Tiba na Ushauri kutoka NHIF Dokta Frank Lekey, akizungumza
na timu ya madaktari Bingwa na madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Shinyanga, kikao cha kuhitimisha zoezi hilo.
ZOEZI
la huduma za madaktari bingwa liliodhaminiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
limehitimishwa mwishoni mwa wiki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga.
Katika zoezi hilo la siku tano jumla ya wagonjwa 740 wamepata huduma na wagonjwa 24 wamefanyiwa upasuaji.
Akizungumza
katika mkutano wa madaktari na timu ya uendeshaji ya hospitali hiyo
kabla ya kuhitimisha zoezi hilo Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri
kutoka NHIF Dokta Frank Lekey amewashukuru madaktari Bingwa kwa uzalendo
wao na kuitolea kufanya kazi katika mazingira magumu.
Aidha
amewahimiza madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
kuendelea kushirikiana katika kutoa huduma kwa wagonjwa na kuhakikisha
kuwa dawa zote muhimu zinapatikana wakati wote.
Naye
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dokta Mfaume Salamu, kwa niaba ya
uongozi wa Hospitali hiyo ameushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) kwa kuwapeleka madaktari bingwa katika hospitali hiyo na kuwapa
uzoefu madaktari wake. Amesema ujuzi waliopata katika kipindi hicho cha
siku tano utawasidia kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa
watakaokuja kupata huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga.
Zoezi hilo sasa linahamia katika mkoa wa Simiyu kuanzia tarehe 06 hadi 10 Julai, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment