HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 9, 2015

FEMA TV SHOW ‘NGUVU YA BINTI’ YATARAJIWA KUANZA RASMI

Mtangazaji wa kipindi cha Fema Tv Show,Rebecca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya uzinduzi rasmi wa kipindi hicho cha Fema Tv Show,itakayo anza rasmi Julai 13 hadi Septemba mwaka huu,huku mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho,Ummy Omary akisikiliza kwa umakini.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa umakini juu ya uzinduzi wa onyesho hilo la Fema Tv.

Na Bakari  Issa, Globu ya jamii.
FEMINA Hip kwa kushirikiana na asasi zingine za kiraia inatarajia kuanza rasmi kipindi chake cha Fema Tv Show Julai 13 Mwaka huu, chenye lengo la kuelimisha jamii kwa ujumla juu ya kuwapa wasichana sauti, nafasi na fursa ya kushiriki masuala mbalimbali ikiwa ni haki ya elimu, haki ya kupata rasilimali pamoja na haki ya kushiriki kwa amani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mtangazaji wa kipindi hicho cha Fema Tv, Rebecca Gyumi amesema katika show hiyo utaona program nyingine zinazohusu masuala ya vijana hususani kuelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2015.
 
amesema kuwa katika kipindi hicho cha Fema Tv Show kitakacho wafikia  vijana wote na jamii nzima pia kitawajibika katika kuibua masuala ya msingi yanayohusu wasichana.

Pia, amesema vipindi hivyo vitarushwa kupitia vituo vya utangazaji vya East Africa televisheni siku ya juma pili saa tatu kamili usiku na na Star TV  kitarushwa siku ya jumatatu saa tatu na nusu usiku.
 
Aidha, amesema Agenda ya Nguvu ya binti mwaka huu inaweza kubebwa na kuwekwa katika ilani za vyama vy asiasa na mipango mingine ya asasi za kiraia inayolenga kuibua masuala ya wasichana na wanawake katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad