HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 6, 2015

BREAKING NYUZZZZZZ.......: BASIL MRAMBA, DANIEL YONNA JELA MIAKA 3

Mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona leo wamekutwa na hatia na katika kesi iliyokuwa inawakabili kwa kipindi kirefu na kuwahukumu kifungo cha kwenda jela miaka mitatu kila mmoja.  Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi Grey Mngonja  ameachiwa huru bada ya kukutwa hana hatia. 

Washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni iliyopata zabuni ya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini ya M/S Alex Stewart.

Hukumu iliyowatia hatiani ni ya wajumbe wawili kati ya jopo la Mahakimu watatu, ambao ni Jaji Samu Rumanyika aliyeanza kusikiliza kesi hiyo kabla ya kuapishwa kuwa Jaji na Hakimu Mkazi Mkuu Saul Kinemela. 
Taarifa kamili inaandaliwa.
 Kaa chonjo.
MAWAZIRI WA ZAMANI, BASIL MRAMBA NA DANIEL YONNA WAKIZUNGUMZA NA MAWAKILI WAO, BAADA YA KUHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MITATU KILA MMOJA. TAARIFA ZAIDI ITAWAJIA BAADAE KIDOGO. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad