Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na
Umoja wa Madereva Tanzania (TADWU)juu ya
usajili waliopata ambao utafanya waweze kuingia mkataba wa waajiri wao na
kuweza kujiunga katika mfuko wa bima ya Afya
uliofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja huo,Clement Masanja, kulia
ni Katibu Mkuu wa chama hicho Abdallah Lubala.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda akikabidhi
Katiba ya Umoja wa Madereva Tanzania
(TADWU) kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo Abdallah Lubala katika hafla iliyofanyika
katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya madereva wakifurahia kupata umoja huo utakaoweka
wazi juu ya ajira ya kazi zao katika katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya
Rombo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda akiagana na
madereva katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.( PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)
No comments:
Post a Comment