Friday, June 26, 2015

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AKUTANA NA TADWU LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na Umoja wa Madereva  Tanzania (TADWU)juu ya usajili waliopata ambao utafanya waweze kuingia mkataba wa waajiri wao na kuweza kujiunga katika mfuko wa bima ya Afya  uliofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam, Kushoto  ni Mwenyekiti wa Umoja huo,Clement Masanja, kulia ni  Katibu Mkuu  wa chama hicho Abdallah Lubala.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda akikabidhi Katiba ya Umoja wa Madereva  Tanzania (TADWU) kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo Abdallah Lubala katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya madereva wakifurahia kupata umoja huo utakaoweka wazi juu ya ajira ya kazi zao katika katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda akiagana na madereva katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.( PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)

No comments:

Post a Comment