Na Bakari Issa
Madjeshi,Globu ya jamii.
Filamu ya Kiswahili ijulikanayo kama Hamu ya Mafanikio ilizinduliwa rasmi jana na Benki
ya DCB katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Filamu hiyo imeandaliwa na DCB Commercial Benki kwa
kushirikiana na Kampuni ya ConsNet,yenye lengo la kuelimisha na kuhamasisha wateja, wadau na umma kwa ujumla juu ya
umuhimu na faida za kufanya shughuli za kibenki na DCB ambazo zinabadili maisha
ya wateja kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo amesema moja ya changamoto zilizopo katika
sekta ya benki ni jamii kukosa elimu ya kutosha juu ya huduma za Kibenki,hivyo
mbali na kujitangaza, DCB imeamua kutoa elimu ya kibenki kupitia Filamu hiyo.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
DCB, Balozi Paul Rupia amewashukuru waandaaji wa Filamu hiyo,ikiwa Bodi ya
Filamu nchini pamoja na wasanii wote walioshiriki kuigiza filamu hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya.
Pia ametoa wito kwa wasambazaji wa Filamu hiyo kuifanya kazi
yao kimakini ili kutimiza malengo na madhumuni ya kuandaa Filamu hiyo.
Washiriki katika Filamu hiyo ni pamoja na Tito Zimbwe,Rose
Ndauka,Jackline Pentezel,Abdul Mhema,Hidaya Njaidi, Gojak na Wasanii wengine
wengi. Baada ya kuzinduliwa Filamu hiyo itaonyeshwa katika maeneo mbalimbali
ikiwemo City Centre,Magomeni,Arnautoglu,Mnazi Mmoja,Tabata,Ukonga,Chanika,Mabibo
na Kariakoo kwa nyakati tofauti kuanzia Julai mwaka huu.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa
DCB, Balozi Paul Rupia akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Filamu
hiyo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana ambapo alitoa wito kwa wasambazaji wa Filamu hiyo kuifanya kazi
yao kwaumakini ili kutimiza malengo na madhumuni ya kuandaa Filamu hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
DCB, Balozi Paul Rupia (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo (kulia) kwa pamoja wakionyesha DVD za Filamu hiyo.
Baadhi ya washiriki na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Filamu hiyo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam,Juni 25,2015.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.
No comments:
Post a Comment