Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amepiga marufuku uchimbaji mchanga
katika mto Mbezi na Kawe Ukwamani kutokana na uharibifu wa mazingira
ambao umesababisha nyumba zilizo kando ya mto huo kubomoka kutokana na
mmomonyoko wa ardhi.
Makonda
alipiga marufuku wakati akizungumza na wananchi walioathiriwa na
mmomonyoko huo alipofika kuwapa pole na kuona jinsi ya kuwasaidia Dar es
Salaam jana.
"Wakati
tunaangalia namna ya kuwasaidi naomba kuanzisha leo shughuli za
uchimbaji wa mchanga katika mto Mbezi ukome na mtu atakaye bainika
anaendelea kuchimba mchanga atachukuliwa hatua za kisheria" alisema DC
Makonda.
Makonda
alisema wataalamu wa Manispaa hiyo watafika katika eneo hilo ili kuona
nini kifanyike kupunguza tatizo hilo kwa siku za mbele kama walivyofanya
maeneo ya Tegeta yaliyokumbwa na mafuriko ambapo kutajengwa karavati
kubwa ili maji yaweze kupita.
DC Makonda akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wakati alipo watembelea waathiriwa hao.
Wananchi wakiwa katika maeneo hayo yaliyoathiriwa na mmomonyoko huo.
Baadhi ya nyumba zilizobomoka kutokana na mmomonyoko huo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
No comments:
Post a Comment