HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 9, 2015

Benki M kushirikiana na Taasisi ya kibiashara ya Marekani Katika kuwasaidia Watanzania wanaosaka ajira

Makamu Mkurugenzi Mkuu wa Benki M, Bi. Jacqueline Woiso (pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati Bank M ikitangaza kushirikiana na Taasisi ya kibiashara ya Marekani ya hapa Tanzania (AMCHAM-TZ) katika kuwasaidia wanaosaka ajira katika kuzikabili changamoto za ajira kisasa zaidi. Wengine pichani toka kushoto ni Makamu wa Rais wa sasa wa AMCHAM-TZ,Bhakti Shah, Mkurugenzi Mkuu wa AMCHAM-TZ, Richard Miles, Bw. David Mbumila kutoka Restless Development na Peter Shiras kutoka Int'l Youth Foundation.
Mkurugenzi Mkuu wa AMCHAM-TZ, Richard Miles (pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kushirikiana na Bank M katika kuwasaidia wanaosaka ajira katika kuzikabili changamoto za ajira kisasa zaidi. 
Bank M leo imetangaza kuwa itashirikiana na Taasisi ya kibiashara ya Marekani ya hapa Tanzania (AMCHAM-TZ) katika kuwasaidia wanaosaka ajira katika kuzikabili changamoto za ajira kisasa zaidi.

AMCHAM-TZ imeandaa semina ya siku moja nzima ijulikanayo kama “DARAJA LA MAFANIKIO” (Bridge to Success) itakayofanyika tarehe 22 Juni mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam. Semina hii italenga kuwasaidia Watanzania kuongeza ujuzi wa namna ya kutafuta kazi na pia watapata mwongozo kutoka kwa maafisa rasilimali watu kutoka katika makampuni na taasisi kubwa zinazoheshimika katika nyanja mbalimbali. Semina hii inatarajiwa kuhudhuriwa na watu wapatao 4,000 wakiwamo wasomi mbalimbali waliomaliza masomo yao hivi punde pamoja na wataalamu mbalilmbali.

Akiongea na waandishi wa habari, mkurugenzi mkuu wa AMCHAM-TZ bwana Richard Miles alisema “Tanzania ina nafasi nyingi za ajira ambazo hazijatumika, hususani kwa vijana na wale wanaotafuta ajira kwa mara ya kwanza.

Na bado kuna nafasi za kazi zaidi ya 112,000 zinabakia, hii ni kwa mujibu wa takwimu kutoka katika ofisi ya taifa ya takwimu (National Bureau of Statistics). “Daraja la mafanikio” ni programu ambayo inalenga katika kuwasaidia wanaotafuta ajira katika kutafuta na kuzikamilisha nafasi za ajira zilizopo.


Wahudhuriaji watapatiwa zana mbalilmbali ikiwamo vigezo vya kielectroniki kwa ajili ya kuandaa CVs, jinsi ya kuandika barua za maombi ya kazi, namna ya kuandaa barua za ufuatiliaji wa ajira  na kadhalika.  Pia watapata nafasi ya kukutana na taasisi na NGOs mbalimbali ambazo zinajihusisha na kutoa mafunzo ya utafutaji ajira na fursa”.

Kwa upande wa Bank M ambao ndio wadhamini wakuu, Makamu mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alieleza kuwa “jambo hili ni mojawapo ya mambo ambayo yamo katika sera yetu ya kusaidia jamii, ni jukumu letu kuisaidia jamii, haswa katika miradi na mambo yenye thamani kubwa kama hii kwa kuwa tunaelewa changamoto ya ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa kwa nchi yetu hivi sasa. Tunaamini kuwa kupitia mradi huu idadi kubwa ya watanzania watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kukabiliana na fursa za ajira na kufanikiwa kufikia ndoto zao”.

Semina hii itakamilishwa na majadiliano ya vikundi ambavyo ndani yake watakuwemo wataalamu wanaojishughulisha na mambo ya ajira na mameneja rasilimali watu (HR) wanaofanya kazi hapa Tanzania, ikifuatiwa na kipindi cha maswali na majibu ambapo wale wanaotafuta ajira watauliza na kujibiwa na wataalamu hao.

Pia watahudhuria wafadhili mbalimbali ambao wanajishughulisha na masuala ya ajira, mafunzo na kazi za kujitolea. Semina hii itatolewa BURE kabisa kwa wanaosaka ajira ambao wanatafuta kazi ambazo wamezisomea. Wanaohitaji wanapaswa kujisajili mwanzoni kupitia kwenye mtandao wa www.amcham-tz.com/daraja-reg.

 “DARAJA LA MAFANIKIO” ni moja ya malengo ya AMCHAM katika kuboresha na kuimarisha sekta binafsi hapa Tanzania, kuhakikisha mazingira ya kudumu ya uwekezaji, kusaidia kujenga mazingira ya kibiashara yenye uwazi na usawa, kuzalisha ajira zaidi na kuinua utajiri uliopo nchini mwetu .

Taasisi ya kibiashara ya Marekani hapa Tanzania ilisajiliwa mwaka 2010, na ni taasisi yenye wanachama zaidi ya 125 wa kibiashara ambazo zipo hapa nchini. AMCHAM-TZ ni taasisi inayofanya kazi kwa kujitegemea bila ya kupata msaada wa kifedha kutoka katika serikali yoyote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad