HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 13, 2015

WAKAZI WILAYA YA KAKONKO WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF - KIGOMA

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Rehani Athuman akitoa maelezo mafupi kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii CHF na namna ambavyo ulivyoweza kuwafikia watanzania na kunufaika na huduma za Mfuko huo unaolenga kuboresha afya za wananchi hususani wenye kipato cha chini na cha kati.
Katibu tawala wilaya ya Kakonko Bi.Zainab Mbunda akifungua Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Afya ya Jamii CHF uliofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko huo wa hiari ambao unawawezesha kupata huduma za matibabu kwa muda wa mwaka mzima baada ya kujiunga na kuchangia kiasi cha shilingi elfu kumi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko Bi.Jaina Msangi akizungumza namna ambavyo Halmashauri inavyosimamia Mfuko huo wa CHF na kueleza kuwa wamekuwa wakihamasisha Jamii kujiunga na Mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma za Afya.  
Baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya waliohudhuria katika Mkutano huo wakiwemo Madiwani,Watendaji wa vijiji,Kata na Vitongoji,Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa,Mashirika,Asasi mbalimbali na Wazee Maarufu wa wilaya ya Kakonko.
Picha ya pamoja. (Picha zote na  KAPIPIJhabari.COM)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad