HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 24, 2015

NOAH YAPARAMIA MTI MAKUTANO YA MTAA WA SAMORA NA SHABAN ROBERT, JIJINI DAR

 Jioni ya leo katika Makutano ya Mtaa wa Samora na Shaban Robert, Gari moja aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 988 BWL iliyokuwa ikitokea upande wa Hospitali ya Ocean Road ilijikuta ikiparamia moja ya mti uliopo kando kando ya barabara hiyo wakati ikijaribu kuikwepa gari nyingine aina ya Toyota Rav4 yenye namba za usajili T449 DDX iliyokuwa ikitoka upande wa Makumbusho ya Taifa huku zote zikiwa kwenye mwendo kasi. hali hiyo ilileta taharuki na mshangao mkubwa kwa watu waliokuwepo eneo la jirani na tukio hilo, hasa kutokana na mwendo kasi waliokuwa nao madereva wa magari hayo. hali hii imekuwa ni desturi ya madereva wengi hapa mjini, hasa inapokuwa siku za mapumziko ya wiki kama leo.
 Hivi ndivyo ionekanavyo Noah hiyo baada ya kuparamia mti huo hapo pembeni.
Mashuhuda wakiwacheki kwa mshangao madereva wa magari yote mawili, wakati wakidiskasi namna ya kufanya, maana mambo ndio yashaharibika hivyo hasa kwa mwenye Noah.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad