HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 11, 2015

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA AZINDUA MKAKATI WA USAJILI NA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO WA MWANZA

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano Mkoa wa Mwanza. Mkakati unalenga kusogeza huduma za Usajili na vyeti vya kuzaliwa katika maeneo wanayoishi na huduma hiyo kutolewa bila ya Malipo.
Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto wenye Umri Chini ya Miaka Mitano wa Mkoa wa Mwanza.
Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akikabidhi Cheti cha Kuzaliwa kwa Mzazi wa mtoto Irine Leon (aliyebebwa), Bw Leonidas Rwehumbiza wakati wa uzinduzi wa Mkakati huo.
Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya Wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mkakati huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad